TRA

TRA

Wednesday, August 17, 2016

Balozi wa Israel Atembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Na John Stephen
Dar es Salaam, Tanzania. Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan LEO ameitembela Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kuahidi kutoa mafunzo kwa wataalamu wa taasisi hiyo.
Balozi huyo ametembelea chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na vyumba vya upasuaji pamoja na kuwaona wagonjwa wodini.
“Nimefurahishwa kusikia kuna madaktari ambao wamesoma Israel na ninapenda kuwaahidi kuwa Serikali yangu itaendelea kuisaidia tasisi hii, lakini sitatoa hela,” amesema LEO.
Pia amesema kuwa anafarijika kuona shughuli za kitabibu zinazofanywa na taasisi hiyo kwa kuwa amekuwa akitaka kwenda kuitembelea lakini hakuwahi kupata nafasi hivyo amefurahi kupata fursa  hiyo.
Wakati huo huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema wanakabiliwa na upungufu wa wataalamu sawa na asilimia 50.
“Tunahitaji wataalamu 278, sasa tuna wataalamu 147 kwa mfano tuna wauguzi 96, mahitaji halisi ni wauguzi 150,” amesema Profesa Janabi.
Katika hatua nyingine, Profesa Janabi amesema hospitali hiyo tayari imewafanyia upasuaji zaidi ya watoto 600 kuanzia mwaka jana hadi sasa.
Profesa Janabi amesema taasisi hiyo imewekeza zaidi katika kununua vifaa tiba vya kisasa na kuwawezesha madaktari na wauguzi kupata mafunzo kutoka nje ya nchi ikiwamo Israel.
 Amesema kuwa mpango huo umesaidia wagonjwa wengi kufanyiwa upasuaji  ambao umekuwa ukifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.
Baadhi ya wageni waliowahi kutembelea taasisi hiyo ni mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania, mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria na mchezaji wa kimataifa, Nwankwo Kanu na madaktari kutoka  nchi mbalimbali ambao wamekuwa wakishiriki katika upasuaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kulia) akimkaribisha Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan wakati alipotembelea taasisi hiyo LEO.
 Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akisikiliza ripoti ya shughuli za kitibabu zinazotolewa na taasisi hiyo kutoka kwa Profesa Mohamed Janabi.
 Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kulia) wakiingia katika chumba cha upasuaji LEO katika taasisi hiyo.
  Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji JKCI, Dk Bashir Nyangasa akifafanua jambo kwa balozi huyo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
 Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akizungumza na madatari, wauguzi na wataalamu wengine wa taasisi hiyo
 Madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wakimsikiliza Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan kwenye taasisi hiyo.
 Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan (kulia) akisaini kitabu cha wageni kabla ya kupata taarifa fupi ya taasisi hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi.
 Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akizungumza na madatari, wauguzi na wataalamu wengine wa taasisi hiyo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza kwenye mkutano huo
  Dk Peter Kisenge akimkabidhi zawadi balozi huyo
Wafanyakazi wa taasisi hiyo wakiwa katika picha pamoja na mgeni huyo. Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger