|
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akikagua Shamba la Mahindi kwenye Kijiji cha Nyang'uku . |
|
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leornad Kiganga Bugomola akikagua Shamba
la Uele kijiji cha Nyang'uku wakati wa ziara ya kutembelea wakulima
Mashamba. |
|
Mkuu
wa Wilaya ya Geita na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakiwa
kwenye Shughuli za kuangalia namna ambavyo wakulima wameitikia kulima
kilimo ambacho kinastahimili ukame. |
|
Diwani wa Kata ya Nyang'uko Elias Ngole akiwatambulisha Viongozi ambao walikuwa wameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Geita. |
|
Wana
Kijiji wa Kijiji cha Nyang'uku wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Geita
wakati alipokuwa akiwasisitiza kuendelea na shughuli za kilimo kwa
kulima mazao ambayo yanastahimili ukame. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wanakijiji wa Nyang'uku. |
|
Shamba la Mtama likiwa limestawi. |
|
Mkuu
wa Wilaya akiwa na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita
pamoja na madiwani wakati wa kuzungukia mashamba Kwenye vijiji vya
Nyang'uku,Ibanda na Bungwangoko. |
Serikali ya
Wilaya ya Geita ,inatarajia kujenga
mradi wa Bwawa la Maji kwaajili ya
Kilimo cha umwagiliaji kwenye vijiji vya
ibanda kata ya Kanyara Chabulongo na Mkoba kata ya Bungwangoko ambapo utaghalimu jumla ya kiasi
cha Sh,Bilioni mbili na nusu.
Akizungumza
na Maduka online ,Fundi Sanifu
umwagiliaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Ally Semfukwe,amesema kuwa mradi
ambao unatarajia kujengwa utanufaisha
vijiji vitano ambapo viwili vinatoka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Sengerema
na vingine vitatu kwenye wilaya ya Geita.
“Mradi huu
wa Bwawa la maji naamini wakulima wataweza kufaidika nao kwani ni shughuli
nyingi ambazo watakuwa wakizifanya tukiachana na Kilimo wanaweza kutumia pia
kwaajili kunyweshea mifugo na kwamba kukamilika kwa mradi huo utaghalimu kiasi
cha sh,Bilioni mbili na nusu”Alisema Semfukwe.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Modest Aporinali amebainisha kuwa
eneo ambalo litatumika kwaajili ya shughuli za utengenezaji wa Bwawa
hilo ni zaidi ya Hekari 500 hadi 1000 na kwamba maeneo hayo ni makazi ya watu
na mradi huo ni wa serikali kuu ambapo wataangalia ni maeneo gani ambayo ni makazi
ya watu kwaajili ya kuwalipa fidia wale ambao watakuwa wamefikiwa na mradi.
Mkuu wa
Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amezungumza na wananchi wa kijiji chA Ibanda
kata ya Kanyara wakati wa ziara yake ya kuzungukia kwenye kata ya
Nyang’uku,Kasamwa ,Bungwangoko na Kanyara ambayo ilikuwa na lengo la kuangalia
kilimo cha Mtama,Mhogo pamoja na pamba,wananchi hao mradio huo ukikamilika
utaleta faida kwani awatakuwa wa kusubilia Msimu wa Mvua na kwamba maji
yatapatikana muda wote pindi wanapoitaji kufanya shughuli za kilimo.
Hata hivyo
pamoja na Mradi huo kuwa ni wamanufaa kwa wakulima ,baadhi ya wakulima wa
kijiji cha Ibanda wamepinga Hatua hiyo na kusema kuwa wao wameshazoea kilimo
cha zamani na kwamba yawezekana kisiwe na tija kwao kutokana na kwamba wanaweza
wakajikuta wakilipia ghalama za kunyweshea mifugo yao.
Mradi wa umwagiliaji
kama utakamilika unatarajia kuwanufaisha zaidi ya wananchi laki moja kutoka
kwenye vijiji vitano.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
No comments:
Post a Comment