Askari akiwa amewakamata Viongozi wawili wa Serikali ya Kijiji waliokuwa wakituhumiwa kwa ubadhirifu wa viwanja.
Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndugu Japhet Muogopeni Mnyagala akizungumza mbele ya Wananchi .
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera akizungumza na Wananchi wa Vitongoji vya FrankWeston na Umojavilivyokumbwa na mgogoro wa ardhi.
Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera, amewatia mbaroni Viongozi wanne wa Serikali ya vijiji kwa kosa la usimamizi mbovu wa ardhi katika Vitongoji vya Umoja na Frank Weston katika kata ya Nanjoka Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.Akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Wilaya Bw. Yahaya Issa Abdallah alimueleza DC. Homera kuwa Vitongoji vya Umoja na Frank Weston vimekumbwa na mgogoro wa ardhi kati ya Wenyeji, Wageni na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya Tunduru kwa muda mrefu.
Aidha
Serikali kupitia Idara ya Ardhi na Maliasili Wilaya, iliwapimia ardhi
Wananchi toka 11/08/2014 lakini ikabainika kuwa mpaka 30/06/2016 bado
Wananchi hawakupewa maeneo yao na kuna baadhi ya Wafanyakazi wa
Halmashauri pamoja na Wageni wapo kwenye orodha ya Wananchi wanaopaswa
kugawiwa Viwanja.
Akihutubia
kwenye mkutano huo wa hadhara, uliyofanyika katika Shule ya Msingi
Umoja, DC Homera aliwaeleza Wananchi kuwa wasiwe na shaka,kwa sababu
Serikali ipo upande wao na hakuna atakaye dhurumiwa haki yake, alisema
“Namtaka Mhasibu wa Ardhi na Maliasili alete orodha ya waliolipia Ardhi
maeneo ambayo siyo ya wakazi, na ambao ni Watumishi wa Halmashauri
wafutwe kwenye orodha hiyo na warejeshewe fedha zao”.
Mfano,
kuna baadhi ya watumishi wa Idara ya Ardhi na Maliasili,ambao wamefanya
ujanja ujanja kinyume cha sheria kwa kuwaweka watoto wao kwenye
orodha,na majina yao yameorodheshwa hapa,hivyo hatua za kisheria na
taratibu zitafanyika kuondoa huu mgongano ambao umejitokeza katika hili
pia.
Kama
vile haitoshi ikabainika kuwa k kuna baadhi ya Viongozi walikusanya
fedha za wananchi wapatao 522 na kutowapa risiti,jambo ambalo ni
hujuma za wazi kabisa za kuikosesha Halmashauri ya Tunduru Mapato na
kupelekea fedha kuwa mikononi mwa wajanja wachache.Aidha
aliwataka Wafanyakazi wa Idara ya Ardhi na Maliasili kujieleza ni kwa
nini wamewagawia watu ardhi ambao sio wakazi? kwa nini wamefanya
udanganyifu wa kuwa milikisha ardhi Watumishi wa Halmashauri kwa njia za
rushwa? na kwa nini wananchi zaidi ya 522 hawajapewa maeneo yao kwa
zaidi ya Miaka Miwili?
Kwa
upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili wa Wilaya ndg. Japhet
Muogopeni Mnyagala alikiri kufanya kosa,lakini pia alimuakikishia Mkuu
wa Wilaya ndani ya wiki moja wananchi wataanza kugawiwa viwanja na zoezi
hilo litaanza (leo).
Mkuu
wa wilaya aliwaagiza askari wakamate viongozi walio kuwa wasimamizi wa
upimaji wa maeneo katika vitongoji vya Umoja na Frank Weston ambao ni
Mohammed Dumsala, Matola Limelime, Halid Daud na Tekla Damas.
SHARE
No comments:
Post a Comment