Hii ni
zawadi ya heshima (tuzo) iliyotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania
na kukabidhiwa kwa mshindi wa kwanza,Mwanafunzi wa darasa la sita kutoka
shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent.

Mkurugenzi
Mkuu kutoka kampeni ya Puma Energy Tanzania Ltd,Philippe Corsaletti
akimkabidhi tuzo/zawadi ya Begi na cheti mwanafuzi wa darasa la sita
kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent baada ya kuibuka mshindi
wa kwanza katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya
kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es
Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma
Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi
Bunge.
Mashindano
hayo yalihusisha shule kumi kwa upande wa Dar Es Salaam ambazo ni
Mwananyamala, Kisutu, Bunge, Kisiwani, Mchangani, Mnazini, Mwananyamala,
Mikocheni, Mtendeni, Kisutu, Kisiwani na Ugindoni,Shule nyingine tatu
ni kutoa mkoa wa Geita ambazo zitashiriki na mchakato wa kuwapata
washindi,matokeo ya washindi wa mwisho yatatangazwa wakati wa kilele cha
cha wiki ya Usalama barabarani ambayo inatarajia kufanyika hivi
karibuni.
Mwanafuzi
wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent akilia
kwa furaha mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Kilele cha
shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika
shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi
iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo
katika viunga vya shue ya msingi Bunge.
Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga pamoja na
Waandaji kutoka kampuni ya Puma Energy Tanzania na AMEND wakitafuta
washindi watatu wa shindano la uchoraji katika masuala mazima ya
kuhamasisha usalama barabarani 2016.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment