TRA

TRA

Thursday, May 4, 2017

Asante Waziri Mwakyembe

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Niliposikia Waziri wa habari, Dk. Harrison Mwakyembe, amepiga marufuku vyombo vya habari kusoma magazeti asubuhi, nilitafakari mambo machache. 

 Biashara ya magazeti haitakuwa ile ile tuliyoizoea. Kuna kile wenzetu wanakiita 'common denominator.


   Waziri mwenye dhamana na habari, Dk Harrison Mwakyembe

Tatizo ni kwamba tulifikiri na bado tunafikiri tuko kwenye biashara ya MAGAZETI kumbe tuko kwenye biashara ya HABARI kwa namna ile ile ambayo KODAK CAMERA walidhani wako katika biashara ya KAMERA kumbe walikuwa kwenye biashara ya PICHA. 

Hawakukumbuka kuwa KAMERA ilikuwa ni nyenzo tu ya kupata PICHA na wala yenyewe si PICHA. Kwa njia hiyo hiyo, GAZETI ni nyenzo tu ya kupitishia HABARI lakini lenyewe (gazeti) si HABARI. 

Ikipatikana njia bora zaidi wanaachana na ile ya awali, na sasa inaonekana imepatikana njia bora zaidi. Teknolojia inabadilika kwa kasi ya mfano ambao haukuwahi kuwapo tangu kuumbwa kwa ulimwengu. 

Hilo agizo la Waziri Mwakyembe laweza kuwa ama sahihi au si sahihi, lakini halina manufaa sana kwa wakati huu wa kasi ya teknolojia.

Social media sasa ina nguvu kuliko MAINSTREAM MEDIA. Kama tamko la Waziri limelenga kuokoa poromoko la biashara ya magazeti, basi ni tamko 'linalofaa' lililokuja wakati 'usiofaa.' 

Tangazo limechelewa, lakini hata lingewahi lisingesaidia chochote. Tunaishi katika enzi tofauti na nyingine yoyote katika historia ya ulimwengu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger