Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bibi. Nuru Millao (kushoto) alipowasili katika banda la Chama
cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) katika viwanja
vya Nanenane John Mwakangale jana Jijini Mbeya. Katikati ni Mwenyekiti
wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili
Mwenyekiti
wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili (wapili kulia) akitambulisha baadhi ya
wajumbe wa TAJATI kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa alipowasili katika banda la Chama cha
Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) katika viwanja vya
Nanenane John Mwakangale jana Jijini Mbeya kwa ajili ya kuzindua chama
hicho
Mwenyekiti
wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili (kushoto) akimuonyesha Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa picha
yenye sura ya kufanana naye iliyochorwa na mmoja wa wanachama wa TAJATI
baada ya kuzindua chama hicho jana Jijini Mbeya katika viwanja vya
Nanenane John Mwakangale. Katikati ni mke wa Waziri Mkuu mama Mary
Majaliwa
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
akipokea zawadi ya saa ya uzinduzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Utalii na Uwekezaji (TAJATI) kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (wapili kushoto)
baada ya kuzindua chama hicho jana Jijini Mbeya katika viwanja vya
Nanenane John Mwakangale. Watatu kushoto ni mke wa Waziri Mkuu mama Mary
Majaliwa
Moja
ya burudani iliyokua ikiendelea kati banda la Chama cha Waandishi wa
Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) jana Jijini Mbeya katika viwanja
vya Nanenane John Mwakangale.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
akihutubia wananchi (hawapo pichani) walioshiriki maonyesho ya nanenane
kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini jana Jijini Mbeya katika viwanja
vya Nanenane John Mwakangale.
:
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.
Nuru Millao (wapili kushoto) akizungumza na viongozi wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI), alipowasili katika
banda lao katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale jana Jijini Mbeya.
Chama hicho kilizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
Katibu
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) Bw.
Venansi Matinya (kushoto) akielimisha umma uliotembelea banda la TAJATI
baada ya chama hicho kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa jana Jijini Mbeya
katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale.
SHARE
No comments:
Post a Comment