Mkuu wa kitengo cha biashara Kampuni ya Maxmalipo Bw.Deogratius Lazari Akifafanua Jambo kwa Waandishi wa habari na Kushoto ni Mkuu wa uendeshaji Kampuni ya Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi
Msemaji wa Kampuni ya Undeshaji wa mabasi ya Mwendo haraka Bw. Deus Bugaywa (Kushoto) Akifafanua Jambo kwa wanahabari na Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya Maxmalipo Bw.Ahmed Lussasi.
Kuanzia sasa wasafiri
wenye kadi maalumu za Usafiri (Dart card) wameongezewa njia mbadala za kuweka
salio katika kadi zao za Usafiri kwa kuwatumia mawakala wa Maxmalipo. Mteja
mwenye kadi hii ya usafiri anaweza kufika kwa Wakala yeyote wa Maxmalipo na kuweka
salio kiasi chochote kwenye kadi yake.
Akiongea kwenye uzinduzi
huu afisa Mwendesgaji mkuu wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi Amesema “ Lengo kubwa
la kampuni ya Maxcom Africa imekua ni kujenga na kutengeneza mifumo imara na
madhubuti ambayo inalenga kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya
kielektroniki pia kusimamia na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa
kutumia mifumo ya Kielektroniki. Bw. Ahmed ameendelea kuelezea kwamba
Tangu Mradi huu wa Mwendo kasi umeanza kumekua na maboresho
mbalimbali na mbinu za kitaalamu zinazopelekea kukua kwa makusanyo, kuepusha na
kudhibiti upotevu wa Mapato na kuhakikisha kuna uwazi wa hali ya juu katika
utoaji wa taarifa za makusanyo (Real time Revenue reporting)”
Naye Msemaji wa kampuni ya
undeshaji wa Mabasi haya ya Mwendokasi Bw. Deus Bugaywa Ameelezea kwa
Ufupi mafanikio kampuni iliyo yapata kwa kutumia mifumo hii ya kielektroniki
moja ikiwa ni uhakika wa mapato, ukuaji wa mapato pamoja na usalama wa fedha
zao”.
Deus ameongeza kwa kusema “ Naweza kuwadhihirishia kwa ushirikiano huu
tulio nao na Maxmalipo katika mradi huu umeleta Mageuzi makubwa katika sekta ya
usafirishaji nchini kwetu barani Africa na Duniani kwa ujumla; Huu ndio mfumo
pekee unaowezesha watu kuweka salio katika kadi zao kupitia MItandao ya simu na
ndio mfumo Pekee uliokua kiteknolojia ndani ya muda mfupi Zaidi, na leo salio
na ticket vinaweza kupatikana kwa mawakala waliopo hata mitaani (hawa wa
Maxmalipo). Ni pongezi kwa Maxmalipo kama kampuni ya kitanzania kwa kufanya
haya, lakini Zaidi Tutoe shukrani zetu kwa serikali kwa kuunga mkono Jitihada
hizi katika sekta nzima ya usafiri.
Naye Mkuu wa Kitengo cha
biashara katika kampuni ya Maxmalipo – Bw. Deogratius Lazari , amwewaambia wana
habari kwamba Maxcom Africa ina Zaidi ya mawakala 15000 nchi nzima ambao
wamewezeshwa kutoa huduma hii kwa watumiaji wa kadi hizi za mwendo haraka. Bw
Deogratius ameainisha pia kwamba Mawakala hawa wa Maxmalipo wapo jirani na
makazi ya watu hvyo wasafiri wanaweza kujipatia huduma hii kabla ya kufika
kwnye vituo vya mabasi ya mwendo haraka.
Kufuatia Uzinduzi huu kampuni ya Maxcom
Africa inatarajia kupungua kwa foleni za abiria kwenye vituo vya mabasi ya
mwendo hasa wale wanaokua wakihitaji kuweka salio kwnye kadi zao pia wanatarajia kuongezeka kwa Ajira katika sekta isiyo rasmi kwa watanzania wengi kuchamgamkia fursa ya kuwa mawakala wa Maxmalipo ambayo itawaongezea kipato.
Maxcom Africa imekua ni Moja ya Kampuni za Kitanzania iliyofanikiwa sana katika uwekaji wa mifumo madhubuti ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato hapa Tanzania hasa katika miradi mikubwa ikiwamo huu wa mabasi ya Mwendo Kasi, TRA, Vivuko, Mahospitali (Moi) na kwenye Kodi za halmashauri
SHARE
No comments:
Post a Comment