Wachezaji
wa timu ya moro kids wakishangilia baada ya kunyakua kombe la
mashindano ya Airtel Rising Stars kwa kuifunga timu ya Angrikana 1-0
katika uwanja wa Jamhuri Morogoro jana.
Kapteni
wa timu ya Moro Kids Abdul Rashid akipokea kombe la mshindi wa kwanza
wa mashindano ya Airtel Rising Stars kutoka kwa mgeni rasmi ambae ni
Meya wa Manispaa ya Morogoro pascal kihanga, Moro Kids imenyakua kombe
hilo baada ya kuifunga timu ya Angrikana 1-0.
Mchezaji
wa timu ya Moro Kids Ibrahimu Ally mwenye jezi nyeupe wakiwania mpira
na mchezaji wa timu ya Angrikana Baraka Omary katika mchezo wa fainali
ya Airtel Rising Starkwenye uwanja wa Jamhuri Morogoroo. Moro Kids
ilinyakua kombe hilo kwa ushindi wa 1-0.
Mshambuliaji
wa timu ya Angrikana Saidi Mohamed akidhibitiwa kikamilifu na beki wa
timu ya Moro Kids Ibrahim Yohana katika pambano la fainali ya Airtel
Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo moro kids
ilinyakua kombe hilo baada ya kushinda 1-0.
Timu
ya vijana ya Moro Kids imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kufanya kazi
ya ziada na kuishinda timu ngumu ya Angrikana 1-0 katika mchezo wenye
upinzani mkali uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana.
Goli
hilo la ushindi liliwekwa kimiani na mshambuliaji machachari Nyamawi
Juma katika dakika ya 22 baada ya kuwazidi mbio walinzi wa Angrikana na
kuachia shuti kali lililotinga wavuni. Goli liliibua nderemo na vifijo
kutoka kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushangilia timu yao.
Angrikana
walijibu mapigo kwa kufanya mashambulizi mfululizo ambayo hata hivyo
hayakuweza kuzaa matunda. Kipingi cha pili walikianza kwa matumaini ya
kupata goli la kusawazisha lakini hadi dakika ya mwisho matokeo yalibaki
kuwa 1-0.
Akikabidhi
kikombe kwa washindi, Meya wa manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga
ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwapongeza Morogoro Kids kwa mafanikio
makubwa na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwa kujituma huku
wakifuata maelekezo ya walimu wao. “Kwa kufanya hivyo kutawaweka katika
nafasi nzuri ya kutimiza ndoto zenu za kufanikiwa katika maisha kupitia
soka”, alisema.
Aliwataka
viongozi wa soka mkoani Morogoro pamoja na makocha kuhakikisha
wanachagua vijana wenye vipaji ili kuuwakilisha vyema mkoa wa Morogoro
kwenye fainali za taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kufanyika
jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 6 hadi to 11.
Wakati
wa mechi hizo za mkoa makocha walipata fursa ya kuwatathimini uwezo wa
kila mchezaji na kuchagua vijana wenye vipaji kuunda kombaini ya mkoa.
Mikoa mingine ambayo tayari imeshaunda vikosi vyake ni kwa fainali hizo
ni Ilala, Kinondoni, Temeke and Mwanza.
Fainali
hizo za kila mwaka itazikutanisha timu za wavulana na wasichana kutoka
mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke. Washiriki wengine
watatoka Mwanza, Morogoro, Mbeya, Lindi, Arusha na Zanzibar.
SHARE








No comments:
Post a Comment