TRA

TRA

Monday, August 15, 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afanya ukaguzi wa kushtukiza kituo cha CHESA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY- (CHESA) kilichopo Upanga, Wilayani Ilala, jijini Dar es salaam.
Ziara hiyo ya kushtukiza inafuatia baada ya hatua ya Naibu Waziri huyo wa Afya Dk.Kigwangalla kuendelea kufanya ukaguzi wa Asasi mbalimbali zisizo za kiserikali zikiwemo NGO’s na CBO zenye makosa ya kiutendaji na kimfumo ambayo ni tofauti na taarifa zao katika usajili wa Serikalini na namna ya uendeshaji wa wao.
Mbali na hayo kituo hicho cha CHESA kinashukiwa kuhusika na vitendo vya uhamasishaji wa mahusiano ya mapenzi ya Jinsia moja (USHOGA), ambayo ni kinyume na mila na Desturi za kitanzania pamoja na Katiba na sharia za Nchi.
“Mahusiano ya jinsia moja si kinyume na mila na desturi zetu tu. Bali hata sheria na katiba ya nchi yetu haziruhusu mfumo huo wa kimahusiano” amesema Dk..Kigwangalla
Aliendelea kubainisha kuwa : “Sisi kama Serikali hatujawahi kusaini mikataba yoyote ya kimataifa inayoruhusu ushoga hivyo kwa taasisi yoyote hapa Nchini inayofanya hivyo ni kuvunja sheria za Nchi na inapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria na hata kufutiwa usajili wake” aliongeza Dk. Kigwangalla.
Katika ukaguzi wa kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akiwa ameambatana na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara anayoiongoza, Bw. Julius Mbilinyi pamoja na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Hassan Selengu pia wamefanya ukaguzi katika kituo hicho ili kubaini kama kuna uwepo wa vilainishi vinavyotumiwa na watu wenye mahusiano ya jinsia moja ambavyo hivi karibuni Serikali ilipiga marufuku matumizi yake hapa nchini.
“Serikali ilikifuta kituo cha ‘SISI KWA SISI’ kwa sababu kilihusika na tuhuma za ushawishi wa mahusiano ya jinsia moja ambacho pia wewe ulikuwa Mkurugenzi wake. Sasa tumeamua kuchunguza na kituo hichi ili tujue kama mnahusika na vitendo hivyo ili tuchukue hatua endapo itabainika ama la” ameeleza Dk. Kigwangalla.
Aidha, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amemtaka Mkuu wa upepelezi Bwana Hassan Selengu afanye uchunguzi wa kina katika kituo hicho ili kubaini pesa za misaada katika kituo hicho zinatokea wapi lakini pia ni kubaini kama kituo hicho kinajihusisha na ushawishi wa watu kujiunga na mahusiano ya jinsia moja.
“Tunawasiwasi kuwa mnapokea pesa nyingi na misaada mingi kutoka katika Taasisi mbalimbali lakini pesa hizo zinatumika kuhamasisha mapenzi na mahusiano ya jinsia moja.
Mbali na hayo. taarifa za usajili wa kituo hichi zinakinzana na malengo na miradi inayofanyika hapa. Pia ipo miradi mbalimbali ambayo haijasajiliwa wala hujaitaja katika maelezo yako lakini inafanyika katika kituo hichi” alihoji Dk. Kigwangalla huku akimtajia baadhi ya miradi hiyo ambayo Serikali inaitambua.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
Tazama hapa MO TV, kuona tukio hilo:
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamis Kigwangalla akiwasili katika ofisi za kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY- (CHESA) kilichopo Upanga, Wilayani Ilala, jijini Dar es salaam.
DSC_5718 DSC_5724Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiandika maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA) Bw. John Kashiha wakati alipotembelea katika kituo hicho chenye maskani yake Upanga, Ilala, Jijini Dar es Salaam, leo Agosti 15.2016
DSC_5730Mkurugenzi wa kituo COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA) Bw. John Kashiha akielezea miradi mbalimbali ya kituo hicho kwa Naibu Waziri. (Hayupo pichani).
DSC_5744Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA).
DSC_5764Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu akiwa pamojana wasaidizi wake wakifanya upekuzi katika ofisi za kituo hicho cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA), Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla.
DSC_5774Upelelezi na Upekuzi ukiendelea ndani ya kituo hicho...
DSC_5796Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo na kuwaonyesha moja ya makablasha (file) zilizokutwa hapo ilikusadia uchunguzi kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA).
DSC_5797Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo na kuwaonyesha moja ya makablasha (file) zilizokutwa hapo ilikusadia uchunguzi kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA)
DSC_5818Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimweleza jambo Bwana John Kashiha wakati wa tukio hilo..
DSC_5811Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya nyaraka za taasisi za kituo hicho
DSC_5828
Upekuzi ukiendelea..DSC_5834Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyesha moja ya kijarida kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA)
DSC_5842Upekuzi ukiendelea.. katika ofisi hizo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger