Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi,
(kushoto), akimkabidhi seemu ya vifaa vya michezo, Mkuu wa Kikosi Maalum
cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Rajabu Nyange Bakari, Agosti 25, 2016. Vifaa hovyo ni vya
michezo ya ngumi, mpira wa miguu na mpira wa pete.
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na Judo.
Akikabidhi
vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa
Mfuko huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili
kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini.
“Nyinyi
mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
tunayo furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza
majukumu mazito ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya
lakini pia kuinua vipaji vyenu,” alisema na kuongeza,
“Nichukue
fursa hii kuwahamasisha mjiunge na PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata
kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha maisha yenu kama
ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi na kamwe
hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi.
Akipokea
vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha
Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari,
aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha
wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya
kiuanamichezo.
Baada
ya makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika
michezo ya mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo.
Afisa
Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa
hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es
Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari. NA K-VIS
BLOG/KHALFAN SAID
Afisa
Matekelezo (Compliance), wa PSPF, George Mnasizu, (kushoto), akigawa
vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa
baadhi ya wanamichezo wa Jeshi la Magereza.
Njaidi
akiwa na Mkuu wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kikosi
Maalum cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Rajabu Nyange Bakari,
na wacheza judo wa kikosi hicho wakiwa katika picha ya pamoja na
vipeperushi vya PSPF.
Njaidi akimkabidhi sehemu ya vifaa hicho, Nahodha wa timu ya mpira wa pete (Netball), wa timu ya Magereza Ukonga, Pili Enzi.
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo kocha wa soka wa timu ya Magereza, Sajenti Hassan Mulego.
Njaidi
akikagua timu ya soka ya Magereza Ukonga, ambayo ilimenyana na Kikosi
Maalum cha Magereza Dar es Salaam, wakati wa bonanza hilo la michezo.
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza.
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza.
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza.
Pambano la masumbwi likiendelea.
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akiwa na Mkuu wa Kikosi
Maalum cha Magereza jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza,
Rajabu Nyange Bakari, wakati akitoa nasaha kwa wanamichezo kabla ya
kuanza kwa bonanza hilo.
Nasaha za mgeni rasmi kwa wanamichezo.
Wanamichezo wakishangilia hotuba.
Onyesho la Judo.
Werema
akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo, Kocha na Afisa Michezo
wa Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, Inspekta Francis Tabu.
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza.
Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.
Picha ya pamoja
SHARE




























No comments:
Post a Comment