
Riek Machar alipowasili mwezi Aprili tarehe 26 mwaka huu .
Makamu wa
rais wa zamani wa Sudan Kusini ambaye pia alikuwa kiongozi wa waasi
Riek Machar, amekimbilia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mshirika
wa karibu wa Machar amethibitisha kuwa kiongozi wao amewasili jijini
Kinshasa na anataka kwenda nchini Ethiopia haraka iwezekanavyo.
Machar
alikimbilia mafichoni kutoka mji mkuu Juba baada ya kuzuka kwa mapigano
kati ya wanajeshi wake na wale wa rais Salva Kiir mwezi uliopita karibu
na Ikulu ya rais.
Baada ya
Machar kuondoka jijini Juba na kukimbilia katika eneo lisilofahamika,
rais Kiir alimteua Taban Deng Gai aliyeongoza ujumbe wa upinzani
kufanikisha mazungumzo ya amani kati ya waasi na serikali kuchukua
nafasi yake, uteuzi ambao Machar alipinga na kusisitiza kuwa anaendelea
kuwa Makamu wa kwanza wa rais.
Gai
amekuwa ziarani nchini Kenya wiki hii na akizungumza na wanahabari siku
ya Jumanne jijini Nairobi, alimtaka Machar kuachana na siasa ili
serikali itekeleze ipasavyo mkataba wa amani.
Wiki
iliyopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la
kutuma kikosi cha wanajeshi 4000 cha kulinda amani kutoka mataifa ya
Kenya, Rwanda na Ethiopia kwenda kulinda amani jijini Juba na
kuhakikisha kuwa maeneo ya Umoja wa Mataifa hayavamiwi.
Kiir na
Machar wameendelea kulaumiana kuhusu mzozo mpya uliotokea katika nchi
yao baada ya kuanza kufanya kazi pamoja mwezi Aprili mwaka huu.
Mapigano
nchini Sudan Kusini yaliyoanza rasmi mwezi Desemba mwaka 2013 jijini
Juba, yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine zaidi ya Milioni
2.5 kukimbia makwao. RFI
SHARE








No comments:
Post a Comment