Waziri
wa Mambo ya Ndani nchini Mh.Mwigulu Nchemba leo amewasili mkoani
Katavi,na kufanya ukaguzi kwenye kambi ya wakimbizi ya Katumba ambako
kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea nchi
jirani ya Burundi na baadae kuamua kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009.
Katika
ukaguzi huo, Mh. Nchemba amesema kuwa zoezi la uhakiki linafanyika ili
kuchunguza mienendo yao na uwepo wao kwenye eneo la Kambi, amesema kuwa
kumekuwepo na taarifa za baadhi ya ndugu zetu ambao wamekuwa
wakijihusisha na watu waovu, kufanya vitendo vya kibaguzi na kutoka nje
ya kambi zao na kwenda nchi jirani bila kibali.
Mbali ya kambi ya Katumba, Waziri Mwiguli alitembelea pia kambi ya Mishamo na kuviagiza vyombo vya usalama na kupitia Seririkali za mitaa kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, na kuongeza kuwa Tanzania haina tabia za kibaguzi "moja kati ya sifa kubwa ya nchi yetu ni kushinda vita dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote tangu tulipopata uhuru" alisema Mh.Mwigulu.
"Natoa rai kwa raia wote tuliowapa kibali cha kufanya kazi, kuishi na kuwa raia wa nchi yetu, waache kujihusisha na vitendo viovu na vya kibaguzi. Hatutawavumilia watu ambao tumewakaribisha kwa nia njema hapa nchini na baadae wahatarishe usalama na amani ya nchi yetu" alisema Mh. Mwigulu.
Waziri Mwigulu alikutana na Askari wa jeshi la polisi na idara zake zote na pia ametembelea gereza la mpanda ikiwa ni ziara ya kupata uhalisia wa changamoto zinazokabili jeshi la polisi, Magereza, Uhamiaji na zimamoto kwa kila mkoa,ambapo tayari kwa majawabu ya kudumu.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba akiwapungia mkono wananchi waliopo kwenye kambi
ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa
waliokuwa wakimbizi kutokea nchi jirani ya Burundi na baadae kuamua
kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009
Sehemu ya Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, wakiwa tayari kumsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba.
Waziri
wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba akiwa katika Mazungumzo na
Viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, wakati alipofika kuzungumza
nao.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba akiongozana na viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Katavi, wakati alipotembelea kambi
ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa
waliokuwa wakimbizi kutokea nchi jirani ya Burundi na baadae kuamua
kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba akiwa nje ya Gereza la Mpanda.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia tanuli la matofali.
SHARE
No comments:
Post a Comment