TRA

TRA

Wednesday, September 21, 2016

Magazeti ya Leo Alhamisi

No comments:


 

FINCA yasamehe mikopo yenye thamani ya TZs Millioni 57 kwa wanachama wake walioathirika na tetemeko

No comments:


index
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO,KAGERA
Benki ya FINCA Microfinance imewasamehe mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 57.2 wateja wake 15 waliothibitishwa kuathirika kwa tetemeko la ardhi lililotokea terehe 10 mwezi huu mkoani Kagera.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Kanda wa FINCA Bw. Aluto Hagamu wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu misaada kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani humo.
Bw. Hagamu alisema kuwa dhumuni kubwa la benki hiyo la kufuta mikopo hiyo ni kuwapunguzia mzigo wanachama hao kutokana na athari walizozipata kutokana na tetemeko hilo na kuwawezesha kurudi katika shughuli wanazozifanya ili kujiweka sawa kiuchumi.
Aidha, Bw. Hagamu kwa niaba ya benki hiyo pia wamekabidhi Sukari mifuko 25, mabati bando 5 pamoja na misumari katoni 8 kwa dhumuni kusaidia waathika wa tetemeko hilo.
Akitoa shukran baada ya kupokea misaada hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu alizitaka benki nyingine kuiga mfano wa benki hiyo za kusaidia wanachama na waathirika wa tetemeko la ardhi kwa ujumla. (P.T)

TTCL na TPDC zatoa milioni 30 kusaidia waathirika tetemeko Kagera

No comments:



 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu akipokea msaada uliotolewa na Bodi ya TPDC (kushoto). Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC Balozi Dkt. Ben Moses msaada ambao unalenga kuwasaidia kurekebisha makazi ya waathirika wa tetemeko hilo lililoukumba mkoa huo.Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu (kulia) akimshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Kamugisha Kazaura (kushoto) mara baada ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya saruji ambayo ni sawa na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10.
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
Wafanyakazi na Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wametoa msaada wa Sh. milioni 20 kusaidia kununua vifaa vya ujenzi kwa waathirika wa tetemekola ardhi mkoani Kagera.
Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa huo Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu, Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC Balozi Dkt. Ben Moses amefafanua kuwa msaada huo unalenga kuwasaidia kununua mabati na saruji kwa waathirika wa tetemeko hilo lililoukumba mkoa huo.
“Sisi TPDC tunatoa msaada wetu kama sehemu ya Watanzania na tatizo hili ni letu sote na Watanzania ni wamoja” alisema Dkt. Moses.
Kwa upande wake Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewashukuru TPDC kwa mchango wao na kubainisha kuwa hakuna kitu kidogo katika kutoa na kuwahakikishia wadau wote wanaotoa michango yao kuwa misaada hyote inayotolewa itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na itasaidia kuwarudishia makazi waathirika wa tetemeko hilo.
Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amewataka watu wote wenye mapenzi mema kuendelee kuwachangia waathirika wa tetemeko hilo na waige mifano ya watu na taasisi mbalimbali wanaoendelea kutoa misaada kwa mkoa wa Kagera ili kuwarudishia makazi wananchi walioathirika maafa hayo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Kapuulya Musomba  amesema kuwa huo sio mwisho wao katika kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi, bali wanaendelea kuwahamasisha wadau wa mafuta na gesi yakiwemo makampuni ya ndani na nje ya nchi ili kuwafanya wananchi waweze kuendelea na kazi zao za kila siku kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) nao wametoa msaada wa mifuko saruji 600 ambayo ni sawa na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10 ikiwa ni mchango wa wa kampuni hiyo katika kuwashika mkono na kuwafuta machozi wananchi wa Kagera. (P.T)

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AIPONGEZA TWIGA STARS KWA KUWA MABINGWA WA CECAFA

No comments:


umn

Rais wa Botswana ''amtaka Mugabe kujiuzulu''

No comments:


Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe
Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe
Rais wa Botswana Ian Khama amemtaka mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe kujiuzulu mara moja kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Ameambia Reuters kuwa taifa la Zimbabwe linahitaji uongozi mpya ili kukabiliana na changaomoto za kisiasa na za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.
''Ni wazi kwamba umri wake na hali ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa kutoa uongozi ambao unaweza kulinusuru taifa hilo''.
Bwana Mugabe ameliongoza taifa hilo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Bwana Khama amemlaumu kiongozi huyo kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.
Amesema mgogoro uliopo Zimbabwe umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku wengine wakielekea Botswana ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa Zimbabwe.
Khama anasema kuwa ataondoka afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ,huku akiwashtumu viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda mrefu. BBC

NEC YAANZISHA PROGRAMU ENDELEVU ZA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA

No comments:


nec1
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akizungumza na waandishi wa Habari mjini Musoma kuwaeleza  mkakati wa NEC wa kuwafikia wananchi moja kwa moja  kuwapatia elimu ya mpiga kura.
nec2
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akizungumza na waandishi wa Habari mjini Musoma kuwaeleza  mkakati wa NEC wa kuwafikia wananchi moja kwa moja  kuwapatia elimu ya mpiga kura.
Na. Aron Msigwa – NEC, Musoma
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutekeleza programu endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura ili kuwaelimisha wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura kutekeleza wajibu na  haki waliyonayo  kikatiba ya kupiga kura katika chaguzi zijazo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani wakati akizungumza na waandishi wa Habari mjini Musoma kuhusu mkakati wa NEC wa kuwafikia wananchi moja kwa moja  kuwapatia elimu ya mpiga kura.
Amesema kuwa Tume hiyo imeanza kutoa elimu hiyo kwa kushiriki maonesho na mikutano mbalimbali ukiwemo mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika  mjini Musoma kuanzia Septemba 22 hadi 24 mwaka huu.
“Tumeamua kushiriki kwenye mkutano huu kwa kuwa hawa ni watendaji wa Serikali katika ngazi za mitaa, tumekuja kutoa elimu ya mpigakura kwani suala la elimu tunalipa kipaumbele” Amesema Bw. Kailima.
Amesema Tume  imeandaa programu ya kuwafikia wapiga kura moja kwa moja kwa kuweka mkakati wa kuhudhuria mikutano yote ambayo iko kihalali ikijumuisha ile ya Mawaziri na Naibu Mawaziri , Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya.
Amebainisha kuwa tayari NEC imewasiliana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili iweze kupata ratiba ya vikao vya kamati za ushauri za mikoa na wilaya ili iweze kupata fursa ya kutoa elimu ya mpiga kura ndani ya vikao hivyo.
Aidha, amefafanua kuwa Tume imemwomba Katibu Mkuu TAMISEMI ratiba ya vikao vya Mabaraza ya madiwani ya halmashauri zote nchini kwa lengo la kuwezesha wataalam wa Tume hiyo kutoa elimu ya Mpiga kura.
“Tumemwomba Katibu Mkuu TAMISEMI atusaidie kuweka ajenda ya kudumu kuhusu utaratibu mzima wa uendeshaji wa uchaguzi na uelimishaji wa mpiga kura kwenye vikao vya mabaraza ya Madiwani ambapo maafisa wa Tume walio katika ngazi za halmashauri watapata fursa ya kutoa elimu ya mpiga kura katika vikao hivyo” Amesisitiza.
Ameeleza kuwa NEC imejipanga kupanua wigo wa utoaji wa habari kupitia vyombo vya habari hasa Televisheni,Redio, Magazeti na Mitandao ya kijamii ili kuwawezesha wananchi wengi  kupata  elimu ya mpiga kura na taarifa sahihi kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi na majukumu yake.
“Tumejipanga kutumia vyombo vya habari, kila wiki tutakuwa na taarifa na mada fupifupi zinazohusu mchakato mzima wa uchaguzi kwa maana ya uandikishaji na zoezi zima la upigaji kura kujenga uelewa kwa jamii nzima kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi” Amefafanua.
Amesema kuwa kifungu Na 4 (c) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 kinaelezea wazi kuwa pamoja na mambo mengine Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina jukumu kutoa elimu ya Mpiga kura, kuratibu Taasisi  na watu wenye uwezo wa kutoa elimu ya mpiga kura ili kuongeza uelewa miongoni mwa jamii.
“Tunategemea kuanzia mwanzoni mwa mwezi Oktoba tutatoa tangazo la kuzialika Asasi na taasisi zinazotaka kutoa elimu ya mpiga kura ziwasilishe maombi yao Tume ya Uchaguzi pamoja na zana zao za kutolea elimu ili tuweze kuwapatia kibali cha miezi 6 na baadaye tutafanya tathmini juu ya ufanisi wa kazi wanayoifanya” Amebainisha Bw. Kailima.
Amesema lengo la kuzishirikisha taasisi na Asasi hizo ni kuondoa ombwe lililokuwa linaonekana la utoaji wa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi pekee kwa kuhakikisha elimu hiyo inatolewa kila wakati ili kuongeza uelewa wa wananchi katika chaguzi zijazo.
Aidha, amesema NEC imeandaa mpango mpya wa kuzifikia shule mbalimbali za Sekondari hapa nchini utakaowawezesha wanafunzi wa shule zitakazochaguliwa kuwa na Klabu za elimu ya mpiga kura.
Amesema programu hiyo itaiwezesha Tume kuwaelimisha wanafunzi  waliofikisha umri wa kupiga kura na wale ambao bado hawajafikia umri huo ili kujenga uelewa wao kuhusu elimu ya Mpiga kura.
“Tumeanza program hii kwa kuzitembelea shule mbili za Sekondari za Isange (wasichana) na Shule ya Ufundi Musoma zilizo katika Manispaa ya Musoma, tutaongea na wanafunzi ambao  wamefikia umri wa kupiga kura lakini bado hawajajiandikisha kupiga kura na wale ambao bado hawajafikisha umri wa kupiga kura, tumenalenga kuanzisha klabu ya Elimu ya mpiga kura kwenye shule moja katika kila wilaya ya Tanzania” Amesema.
Amefafanua kuwa kuanzishwa kwa klabu hizo kutawawezesha wanafunzi kujadiliana kwa kina kuhusu mfumo wa uandikishaji wa wapiga kura kwa mujibu wa sheria iliyopo ili kufikia lengo la kuwa na shule moja yenye Klabu ya elimu ya mpiga kura katika kila wilaya  ifikapo Januari 2020.  (P.T)

MHE. JENISTA MHAGAMA: “SERIKALI IMETIBU WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGER BURE”

No comments:


kae1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiangalia athari ya tetemeko katika eneo la Shule ya Msingi Bieju Kata ya Mtukula wakati alipowasili Wilayani Misenyi kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.
kae2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akipokea maelezo juu ya idadi na thamani ya uharibifu katika shule ya Sekondari Mtukula toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Luteni Kanali Denice Filangali Mwila wakati alipowasili Wilayani hapo kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.
kae3
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akiongea na wakazi wa Kata ya Bugandika, Wilayani Misenyi wakati alipofanya ziara Wilayani hapo kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.
Na Benedict Liwenga-WHUSM, Kagera.
SERIKALI imetibu wananchi bure ikiwa ni sehemu ya msaada wake kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Kauli hiyo imetolewa leo Mkoani Kagera na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama wakati alipofanya ziara Wilayani Misenyi kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi.
Mhe. Mhagama ameeleza kuwa, Serikali hadi hivi sasa imewatibu watu zaidi ya 400 kupitia hospitali zake za Wilaya na Mkoa kwa kuagiza madaktari kutoka nchini China ambapo zoezi la kusambaza damu pamoja na dawa za kutosha kwa waathirika lilifanyika na hakuna mwananchi aliyetozwa fedha kama malipo ya huduma hiyo.
“Tuishukuru Serikali yetu kwa kutusadia kupata dawa na damu ya kutosha na tulihakikisha kuwa kila mtu aliyepatwa na tetemeko na kujeruhiwa anatibiwa kwa gharama za Serikali ndiyo maana tuliagiza madaktari kutoka China pamoja na Mwanza ili kusaidia kuwatibu wananchi waliopatwa na majeraha makubwa”, alisema Mhe. Mhagama.
Aliongeza kuwa jumla ya wagonjwa ambao kwa sasa wanaendelea kutubiwa hospitalini ni 23 na ndiyo ambao wamefanyiwa upasuaji mkubwa na hali zao zinaendelea vizuri tofauti ilivyokuwa hapo awali.
Alifafanua kuwa, Serikali haiwezi kumsaidia kila mtu kwani haina uwezo huo lakini inajitahidi kurejesha miundombinu yake na taasisi zake zikiwemo zahanati, shule barabara kwa kushirikiana na wadau wanaojitokeza kuunga mkono juhudi za kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo, hivyo ametaka wananchi kujitokeza na kushirikiana kwa pamoja katika kuwasaidia waliopatwa na tukio hilo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila amesema kuwa katiika Wilaya yake sehemu iliyoathirika zaidi ni Kata ya Minziro ambapo jumla ya nyumba 512 haziwezi watu kuishi,pia nyumba 1,524 zenye nyufa mbalimbali zinazohitaji ukarabati, Taasisi za serikali 91 na taaisis 71 za watu binafsi ikiwemo makanisa na misikiti imeathirika na tetemeko hilo.
Ameongeza kuwa tayari amepata msaada wa Serikali katika tukio hilo kupitia Kamati ya Maafa ni ambapo jumla ya maturubai 520 amepewa kwa ajili ya maeneo mbalimbali, chakula, blanketi 240 ambazo pia zimegaiwa kwa waathirika pia.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo amewataka wananchi wake kutobeza juhudi za Serikali zinazofanywa sasa ambapo amewataka kuridhika na chochote wakipatacho katika kipindi hiki kigumu.
Hivi karibuni siku ya tarehe 10 Septemba, 2016 mkoa wa Kagera ulikumbwa na ukubwa wa nguvu za mtetemo wa ardhi wa tetemeko la 5.7 kwa kutumia skeli ya ‘Ritcher’ ambapo jumla ya watu 17 walipoteza maisha na majeruhi kadhaa ambapo wengi wao wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.  (P.T)

Marekani na Urusi zatupiana maneno juu ya Syria

Published in Jamii
Moja ya malori yaliyoteketezwa
Moja ya malori yaliyoteketezwa
Marekani na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria, pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano.
Wamarekani wamekuwa wakiamini kuwa Urusi ndio iliyoshambulia msafara huo, huku Warusi wakilipinga hilo.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi John Kerry, alitoka nje ya lugha ya kidiplomasia kwa kutumia dhihaka zaidi. Huku mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov akipinga hisia hizo kali kwa kuorodhesha mifano kadhaa kutetea nchi yake. Aidha ametaka pia kufanyika
Licha ya majibizano makali, Urusi na Marekani zilikubaliana kwa pamoja kuongoza mkutano wa mataifa 23, yanayoiunga mkono Syria ambao utafanyika mjini New York, baadaye leo.
Katika hatua nyingine Umoja wa Mataifa umesema unajiandaa kuanza tena kutoa misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyozingirwa nchini Syria, baada ya kusitishwa kwa usambazaji wa misaada kufuatia shambulio hilo.
Mjumbe wa Umoja wa Mnataifa nchini Syria, Staffan de Mistura ameiambia BBC kwamba misafara hiyo ya misaada itaanza katika baadhi ya maeneo lakini kwa uangalifu na tahadhari kubwa. Misaada hiyo amesema haitasambazwa katika eneo linaloshikiliwa na waasi la Aleppo, ambalo limeshambuliwa vibaya. BBC

DC MTATURU: SERIKALI ITAVISAIDIA VIKUNDI VITAKAVYO KUWA TAYARI KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

No comments:


1
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza umakini kwa wananchi waliojitokeza kwenye Kikao cha Mafunzo ya namna bora ya kushiriki katika kilimo chambogamboga na matunda kupitia umwagiliaji

Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo akiwasihi wananchi kutumia njia za kisasa katika kilimo cha umwagiliaji na kufuata taratibu wanazoelekezwa na wataalamu wa kilimo

Baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali sawia na wajumbe washiriki kwenye mafunzo hayo wakifatilia kwa makini Muelimishaji

Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya RIWADE Mhandisi Ayubu Massau, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Moses Msai Mratibu wa RIWADE mkoa wa Singida na Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo

Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe wakifatiliakwa makini mafunzo ya namna bora ya kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia Gree House

Kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Hassan Tati, Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya RIWADE Mhandisi Ayubu Massau, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Moses Msai Mratibu wa RIWADE mkoa wa Singida na Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo

Dc Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo hayo
Na Mathias Canal, Singida
Uongozi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida umeahidi kuvisaidia vikundi mbalimbali ambavyo vitakubali kujihusisha na kilimo cha mbogamboga na matunda (Perishable Crops) sambamba na kilimo hicho kwa kutumia Kitalu Nyumba (Green House).
Kauli ya serikali imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati akifunga mafunzo kwa wajasiriamali, wakulima na wafugaji yaliyoendeshwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya Right Way For Development (RIWADE) kwenye ukumbi wa Mikutano katika Shule ya Sekondari Ikungi na kuhudhuriwa na watu 115 ambao wanatokea katika Kata 24 kati ya Kata 28 zilizopo Wilayani humo.
Katika Mafunzo hayo jumla ya Vikundi 39 vimehudhuria ambavyo vimetakiwa kujishughulisha zaidi kukimbia kilimo cha mazoea ambacho wakulima hulima msimu mmoja hadi mwingine na hatimaye kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji ambacho kinatumia muda mchache kukamilika na kuanza kwa mavuno.
DC Mtaturu amevitaka vikundi hivyo kwa pamoja kutumia vyema fursa ya Makao makuu ya serikali kuhamia Mjini Dodoma kwani itakuwa taswira chanya katika kukuza soko la mazao yao pasina kupata ugumu wa uuzaji.
Amesema kuwa Mkoa wa Singida mara nyingi umekuwa ukitajwa kama mkoa masikini nchini Tanzania kati ya mikoa 10 ambayo ipo mkiani katika maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya wananchi wenyewe kutofanya ubunifu katika kilimo chao jambo ambalo linasababisha uzalishaji mdogo na kupelekea kipato kuendelea kuwa duni ilihali maandalizi ya mashamba ni makubwa.
Mtaturu amesema kuwa wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa serikali katika kukamilisha adhma yake katika uwekezaji na Tanzania ya viwanda kwani endapo watakubali kulima kilimo cha kisasa na kuwa na uzalishaji mkubwa itakuwa rahisi kwa serikali kuanzisha viwanda vya kusindika mazao.
Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya RIWADE ambayo imesajili kwa lengo la kiwasaidia vijana wasio na ajira waweze kufanya kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Mazingira Mhandisi Ayubu Massau alisema kuwa wananchi wanapaswa kufikia kilimo cha kuachana na kuuza mazao yao kwa madalali badala yake kuuza moja kwa moja kwa mtumiaji jambo ambalo litatoa fursa chanya ya mafanikio makubwa katika pato la mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo amepigia chepuo zaidi kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) na kusema kuwa ndicho kilimo pekee chenye uwezo wa kuwatoa wananchi kwenye kadhia ya umasikini kwani kilimo hichp kupitia umwagiliaji wa kisasa unatumia maji machache na matokeo yake ni makubwa kama wakulima watafuata taratibu zote za utunzaji wa shamba.
Massau alisemaMkuwa umefika wakati wa wananchi kuachana na vyama vya kufa na kuzikana badala yake kujihusisha zaidi na vyama vya kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi mbalimbali.
Naye Moses Msai ambaye ni Mratibu wa RIWADE mkoa wa Singida alisema kuwa wakulima wanapaswa kutambua kuwa sekta pekee yenye uwezo wa kuajiri watu wengi na kuwatoa kwenye lindi la umasikini ni Sekta ya Kilimo hivyo ni vyema kufanya kilimo cha kisasa kwani ndicho kitakacho wanufaisha wananchi.
Ametoa fursa kwa wananchi kujiunga na RIWADE kwani watapata fursa ya kuunganishwa na wataalamu ili kuelekezwa namna bora ya kulima kilimo cha umwagiliaji.
Hata hivyo Mjasiriamali na mkulima aliyeshika nafasi ya Kwanza kanda ya kati katika sekta ya kilimo Hassan Tati aliwasihi wakulima hao waliopatiwa mafunzo kuwa mafanikio kwenye kilimo ni makubwa endapo wakulima watafuata taratibu za kilimo na kuwasikiliza wataalamu.
Tati amesema kuwa hakuna ajira nzuri duniani kama kuwekeza kwenye kilimo lakini amewasihi wananchi kuing’ang’ania Asasi ya RIWADE kwani ni taasisi muhimu kwa kila mmoja kwa kujitolea kutoa mafunzo ya kilimo na ufugaji.
Asasi isiyo ya kiserikali ya Right Way For Development (RIWADE) ilianzishwa Mwezi June 2016, ikiwa ni dhima ya kutengeneza na kutoa fursa kwa watanzania wote ili waweze kupata elimu ya ujasiriamali na namna ya kutengeneza mitaji kwa ajili ya ukuaji endelevu wa kijamii na kiuchumi. (P.T)

Monday, September 19, 2016

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA MKOANI MWANZA NA KUAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA ASKARI NCHINI.

No comments:





Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, alipofanya ziara kwenye makazi ya askari ya kigoto yalipopo Kata ya kirumba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza hii leo.

Na George Binagi-GB Pazzo @BMG

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini imeahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazovikabili vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo uhaba wa makazi na sale za askari ili kufanikisha vyombo hivyo kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa.

Waziri anayeshughulikia wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, ametoa agizo hilo hii leo kwenye kikao baina yake na viongozi mbalimbali wa vikosi vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, kilichofanyika kwenye gereza kuu la Butimba Jijini Mwanza.

Amesema jitihada za ujenzi wa nyumba za ghorofa kwa ajili ya makazi ya askari katika miji mikuu ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam zitaenda sambamba na ujenzi wa nyumba za kawaida katika wilaya mbalimbali nchini ili kutatua kero hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Nchemba ametoa onyo la kukamatwa wale wote wanaotoa kejeli kwenye mitandao ya kijamii juu ya utendaji kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini pamoja na askari wanaopata madhara wakipambana na uhalifu, kama ilivyotokea katika tukio la mauaji ya askari lililotokea hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Awali Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, amebainisha baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo kuwa ni pamoja na ukosefu wa makazi ya askari, uhaba wa fedha pamoja na madeni ya askari, ambazo zikifanyiwa kazi zitaboboresha zaidi utendaji wa jeshi hilo.

Waziri Nchemba amefanya ziara ya siku moja mkoani Mwanza, akitokea mkoani Kagera alikoenda kujionea uhalibifu uliotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwanzoni mwa mwezi huu na kuzungumza na watendani mbalimbali wa taasisi za wizara yake, ambapo ametembelea makazi ya askari ya Kigoto na gereza kuu la Butimba Jijini Mwanza, kabla ya kuendelea na ziara yake hapo kesho mkoani Mara.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Kirumba Ilemela Jijini Mwanza (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba (kulia) kwenye makazi ya askari Kigoto Jijini Mwanza. Katikati ni Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi.
Maofisa mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kwenye makazi ya skari Kigoto Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akiwa amembeba mmoja wa watoto kwenye makazi ya askari Kigoto Jijini Mwanza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Afisa wa polisi akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmad Msangi, akizungumza kwenye kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akizungumza kwenye kikao baina yake na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akizungumza kwenye kikao baina yake na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akizungumza kwenye kikao baina yake na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Baadhi ya Maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye kikao baina yao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Baadhi ya Maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye kikao baina yao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Baadhi ya Maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye kikao baina yao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.

BREAKIN NEWZZ!!:- CHADEMA WAMFUKUZA KIGOGO WAO KWA UTAPELI

No comments:



Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA 
By Pamela Chilongola,mwananchi
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema) wilaya ya Temeke kimemfukuza uanachama Diwani wa Kata ya Kurasini ambaye ni  mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa  Mivinjeni , Matiti Togocho
kwa kile walichodai kuwa amekuwa akifanya ufisadi ikiwemo kutengeneza hati za viwanja feki na kujipatia kipato.
 

Mwenyekiti Chadema wilaya hiyo Berdad Mwakyembe amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na makosa ya ufisadi aliyowafanyia wananchi wa kata yake.
 
Mwakyembe alisema diwani huyo ameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake badala yake alikuwa anatumia nafasi yake kujinufaisha huku akiwawakandamiza wananchi wanyonge.
Hata hivyo Diwani Togocho alisema hatozungumzia suala hiko hadi atakapopewa ruhusa kutoka kwa mratibu wa kanda kuongea suala hilo
 
“Unajua aliyeongea mwenyekiti wangu hivyo siwezi kuropoka kitu hadi nisikilize mabosi wangu ambaye mratibu wa kanda,”alisema Togocho.
Source:- Mwananchi/Citizen

Mauzo DSE yashuka kwa asilimia 81

No comments:


Na Ally Daud-Maelezo.
MAUZO katika Soko la Hisa Dar es salaam (DSE) yameshuka kwa asilimia 81 kutoka Tsh. Bilioni 9 mpaka kufikia shilingi bilioni 1.7 kutokana na kushuka kwa idadi ya uuzaji wa hisa kufikia shilingi 340,000 kwa wiki hii.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Afisa Mwandamizi wa masoko wa DSE Bi. Mary Kinabo amesema kuwa mauzo hayo yameshuka kutokana na ukubwa wa mtaji wa soko kushuka kwa asilimia 2.79 kutoka trilioni 21.3 kufikia trilioni 20.7.
Aidha  Bi. Mary amesema kuwa ukubwa wa mtaji kutoka makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha shilingi trilioni 8.2 kutoka wiki iliyopita.
Bi. Mary amesema kuwa licha ya idadi ya mauzo kushuka pia  Benki ya CRDB imeshika nafasi ya kwanza katika kuuza na kununua hisa kwa asilimia 53 ikifuatiwa na kampuni ya Bia nchini TBL kwa asilimia 35 huku kampuni ya Swissport ikishika nafasi ya tatu ya kununua hisa kwa asilimia 3.
Mbali na hayo Bi. Mary amesema kuwa licha ya viashiria vya soko kushuka kwa alama 36.6 baada ya bei za hisa kutoka TBL kushuka kwa silimia 1.08,  viashiria vya huduma za kibenki na kifedha vimepanda kwa alama 3.64 baada ya mauzo ya DSE kupanda kwa asilimia 11.5.

Tuesday, September 13, 2016

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

No comments:


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza sala wakati wa ufunguzi wa kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisema serikali ipo katika uhakiki wa maombi ya maeneo mapya utawala kwa kuangalia vigezo katika kuanzisha maeneo hayo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisema serikali serikali itaendelea kuongeza udahili wa walimu wa sayansi katika vyuo vya elimu ili kuweza kukidhi mahitaji husika.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (kushoto) akimueleza jambo Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo aliwaeleza wabunge kuwa Katiba ya Nchi ibara ya 3(2) inaeleza kuwa mambo yote yanayohusu uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiswa kwa mujibu wa masharti ya katiba na sheria iliyotungwa ba Bunge
Waziri Wizara ya Mmabo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo alisisitiza watanzania kufuata sheria za nchi na iwapo utakiuka jeshi la polisi litachukuwa hatua bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa.
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijini Mhe. John Heche akichangia hoja kuhusu tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati wa kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Mhe. Prof. Anna Tibaijuka akichangia hoja kuhusu tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati wa kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma ambapo mbali na mambo mengine wabunge wamekubaliana kuchangia posho ya siku moja kwa ajili ya wahanga wa tetemeko mkoani Kagera.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakisimama kwa dakika moja kuungana na wahanga wa tetemeko lililotokea mkoani Kagera.
Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akitoa taarifa ya serikali kuhusu tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni Mkoani Kagera. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger