Mgombea
urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ameeleza
mpango wake wa kuwahakikishia usalama wao Wamarekani.
Hata
hivyo hakueleza bayana jinsi utakavyofanikishwa mpango huo, muda
utakaochukua na watakavyogharamika walipa kodi.Trump ambae awali alikuwa
amependekeza kupigwa marufuku kwa muda Waislamu kuingia Marekani ,
ameapa kubadilisha sera za mambo ya nje za nchi hiyo ili kukabiliana na
wanaunga mkono makundi yenye itikadi kali na wasiofuata maadili ya
Marekani.
Katika
hotuba yake juu ya sera za uhamiaji aliyoitoa katika jimbo lenye
ushindani mkubwa la Ohio, Trump amesema Marekani inahitaji kushirikiana
na mataifa yote ambayo yanataka kukabiliana na ugaidi. Mgombea huyo wa
chama cha Republican alisema baadhi ya mapendekezo yake muhimu katika
kukabiliana na hali hiyo ni kuliangamiza kabisa kundi la dola la
kiislamu IS. Amesema Vyombo vya serikali vitahitajika kuwahoji kwa kina
wanaotaka kuingia katika ardhi ya Marekani, kuyafwatilia maisha yao
katika mitandao ya kijamii na hata kuzihoji familia na marafiki zao.
Hata
hivyo Trump hakueleza nguvu kazi itakayohitajika katika kufanikisha
mpango huo. Matamshi yake yanawadia katika wakati mgumu wa kampeini
zake, huku anapojaribu kuwashawishi wamarekani kwanini wampigie kura
dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton.
Hillary Clinton
Katika
hotuba hiyo ya Ohio Trump alionekana kubadili msimamo wake wa awali, wa
kuatka kufanyiwa mageuzi muungano wa kijeshi wa Nato na kuapa
kushirikiana nao.
"Tutafanya
kazi kwa karibu na NATO katika harakati zake mpya za kukabiliana na IS.
Awali nikuwa nisema NATO imepitwa na wakati, kwasababu ilishindwa
kukabiliana na vilivyo na ugaidi,Tangu nitoe kauli yangu,muungano huo
umebadili sera na sasa una kitengo kipya cha kukabiliana na vistisho vya
kigaidi.Na jambo nzuri.”amesema Trump.
Taarifa
nyingine ni kuwa wafungwa15 waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la
Guantanamo nchini Marekani wamehamishiwa katika Umoja wa Falme za
Kiarabu, hii ikiwa idadi kubwa ya wafungwa kuhamishwa kwa wakati mmoja
mnamo miaka ya hivi karibuni.Uhamisho huo unaifanya idadi ya wafungwa
waliosalia katika gereza hilo kuwa 61.Tangu shambulizi la septemba 11,
2011, karibu wafungwa 780 walikuwa wakizuiliwa katika gereza hilo.
Kwa
mujibu wa afisa mmoja wa idara ya serikali 12 miongoni mwa wafungwa hao
waliohamishwa ni raia wa Yemen na watatu ni kutoka Afghanistan.Awali
wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon ilikuwa imetafuta taifa la tatu
kuwapeleka raia hao wa Yemen kutokana na machafuko yanayoendelea katika
taifa lao.DW
SHARE
No comments:
Post a Comment