
Mama Tereza atawazwa kuwa mtakatifu
Maelfu ya watu wameshuhudia ibada ya kutawazwa kuwa mtakatifu, ambapo Papa Francis amemtangaza mtawa Mama Teresa kuwa mtakatifu.
Raia huyo
wa Albania ambaye alifariki mwaka wa 1997 alianzisha shirika la hisani
la kimishenari ili kuwasaidia walala hoi katika mtaa wa mabanda wa
Calcutta nchini India.
Atajulikana kuwa mtakatifu Teresa wa Calcutta.
Waandishi
wnasema kuwa maisha yake yanaenda sambamba na maono ya Papa Francis
kuhusu kanisa linalojikakamua kuwasaidai watu masikini.
Lakini
wakosoaji wanasema kuwa Mama Teresa hakuwasaidia watu waliokuwa wagonjwa
,na alilaumiwa kwa kujaribu kuwabadilisha dini watu masikini wa kabila
la Hindu nchini India kuwa Wakristo.BBC
SHARE








No comments:
Post a Comment