
Na Masanja Mabula -Pemba
NAIBU
waziri wa Habari , Utalii , Utamaduni na Michezo Bi Chumu Kombo Khamis
amewataka vijana kujikusanya na kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali
ili waweze kujiletea maendeleo .
Amesema ,
zipo fursa nyingi ambazo zinaweza kuwakomboa vijana kutoka katika wimbi
la umaskini iwapo watazitumia ipasavyo kwa kukaa pamoja na kubuni
shuhuli za maendeleo .
Kauli
hiyo ameitoa wakati akizungumza na vijana wa Jimbo la Micheweni ambapo
amebainisha fursa hizo kuwa ni sekta ya Michezo ambayo imekuwa ikitoa
ajira kwa vijana .
Aidha
Naibu Waziri amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia
Wizara ya Habari , Utalii , Utamaduni na Michezo itaendelea kuwaunga
mkono vijana wenye nia ya kujiajiri kupitia sekta mbali mbali .
“Zipo
fursa nyingi ambazo ikiwa zitatumika ipasavyo , suala la umaskini kwa
vijana litakuwa ndoto , hivyo naomba mzitumie kwa ajili ya kupata ajira
miongoni mwake ni sekta ya Michezo ” alisisitiza Naibu Waziri.
Mapema
akizungumza katika hafla hiyo , Hamad Mbwana amewataka vijana kuacha
kutegemea aajira kutoka serikalini badala yake wahakikishe wanazzitumia
fursa zilizopo kutengeneza ajira zao binafsi.
Amesema
zama za kutegemea ajira kutoka Serikalini kwa wakati huu zinaweza
kumdumaza kijana , kutokana na serikali kutoa ajira kidogo kulingana na
Idadi ya vijana waliosoma , hivyo fursa pekee ni kujiunga katika vikundi
vya ujasiriamali .
“Ni
lazima tuelewe kwamba vijana waliosoma ni wengi hivyo hawawezi kuajiriwa
wote na Serikali kwa wakati mmoja , hivyo fursa pekee ni kujiajiri
wenyewe kupitia sekta mbali mbali ikiwemo michezo “alifahamisha .
Kwa
upande wao , baadhi vijana wamesema kwamba bado zipo changamoto
zinazowakabili ikiwemo suala la mitaji na kuiomba Serikali kusaidia
kuwapatia taalauma ambayo wataitumia katika kufikia maendeleo
waliyokusudia . (P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment