
Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa mara
nyingine ametimiza ahadi yake kwa kuipeleka nje ya nchi timu ya taifa ya
Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’
ambako itapiga kambi ya utulivu kabla ya kucheza na Congo-Brazzaville
katika mechi ya mkondo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo.
Benchi la
ufundi lilimshauri Rais Malinzi kwamba kambi hiyo ipigwe jijini
Victoria, kwenye Kisiwa cha Mahe nchini Shelisheli. Serengeti Boys
inatarajiwa kuondoka nchini usiku wa kuamkia Jumatatu kwenda Shelisheli
ambako itafanya mazoezi maalumu kwa ajili ya mchezo huo ambao utafanyika
Septemba 18, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hii ni
mara ya pili kwa Malinzi kutimiza ahadi yake kwa wachezaji hao. Kwa mara
ya kwanza aliahidi kuwapa kambi ya nje kama wangewatoa Shelisheli. Timu
kweli ilikwenda Madagascar kabla ya kuivaa Afrika Kusini ‘Amajimbos’ na
kuitoa na kwa sasa inakwenda Shelisheli kujipanga kwa ajili ya kuitoa
Congo-Brazzaville.
Serengeti
Boys ambayo ilipiga kambi Hosteli za TFF, zilizo Karume kwa siku nne
kabla ya safari hiyo na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime
maarufu kama Mchawi Mweusi amesema kwamba anaamini kuwa mchezo ujao
utakuwa mgumu kwa kuwa kila timu itajipanga kuvuka ili kucheza fainali
hizo.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment