
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akiangalia muonekano wa Jengo jipya la makazi ya
Mhe Waziri Mkuu lililopo Mlimwa Dodoma wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana.

Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagam (katikati) akipewa maelezo ya eneo la Makazi Mapya
ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya
Ujenzi Bw. Keffa Chana alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba
02, 2016 Mlimwa Dodoma.

Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akitoa baadhi ya maagizo kwa viongozi wa Serikali
wakati wa ziara yake katika Jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Septemba 2, 2016 wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe.
Jordan Rugimbana.

Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akiangalia muonekano wa jengo jipya la Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alipofanya ziara yake tarehe 02 Septemba, 2016
Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Na. MWANDISHI WETU.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (mb) amesisitiza kuwa dhamira ya
Serikali kuhamia Dodoma ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka minne
hatua kwa hatua.
Akizungumza
na waandishi wa habari Septemba 2, 2016 wakati wa ziara yake eneo la
Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim yaliyopo Mlimwa Dodoma,
Waziri Mhagama alisema “Watanzania wawe na amani, dhamira yetu iko
vizuri na kama Mhe. Rais alivyosema na tunawahakikishia kwamba ndani ya
kipindi hicho sisi tumeshajipanga kuhamamia mkoani Dodoma hatua kwa
hatua”.
Waziri
Mhagama alieleza kuwa shughuli za maendeleo hazitosimama kwa kuzingatia
mipango iliyopo na bajeti ya Serikali, “Niwatoe wasiwasi kwamba mipango
yote ya maendeleo haitosimama na shughuli zote za maendeleo hazitozuiwa
na ujio wa Serikali mkoani Dodoma zitafanyika kama zilivyopangwa na
tutaendelea kuyafanya hayo kwa kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya mwaka
2015 Ibara ya 151 tumesema tunahamia Dodoma na tutafanya
hivyo”.Alisisitiza Mhagama
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi
kutekeleza usimamizi wa maagizo ya Waziri ili kukamilisha ujenzi wa
barabara kwa wakati “kwa upande wa mkoa kazi iliyobaki ni kuhakikisha
kuwa ujenzi wa barabara unakamilika na tutakutana na Wakala wa Barabara
(TANROADS), Mamlaka ya Ustawishaji Mji (CDA) na Manispaa ili kuona
shughuli hii tunaifanyeje kwa kutekeleza maagizo hayo ikiwa ni sehemu ya
majukumu ya mkoa.”
Aidha,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana alimshukuru Waziri Mhagama kwa
kutembelea maeneo ya makazi mapya ya Mhe. Waziri Mkuu na Jengo la Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,”Namshukuru Mhe. Waziri Mhagama, Manaibu
Waziri na Ofisi yote ya Waziri Mkuu kwa ziara hii na kukamilisha awamu
ya kwanza ya ujenzi wa Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu.” (P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment