TRA

TRA

Monday, October 31, 2016

Mkurugenzi wa FBI matatani

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Bildkombo James Comey und Hillary Clinton (Getty Images/AFP/Y. Gripas/J. Sullivan)
Seneta wa juu kabisa wa chama cha Democrat, amesema Mkurugenzi wa FBI James Comey anaweza kuwa amevunja sheria kwa kutangaza kubaini barua pepe mpya zinazoweza kuwa muhimu kwa uchunguzi dhidi Hillary Clinton
Katika barua yake kwa Comey, kiongozi wa kundi la wachache Harry Reid, seneta wa Nevada amemtuhumu kiongozi huyo kwa kuwa na undumilakuwili kwa kuwa na nia ya kudhibiti wito wa Democrat kujadili kile kinachoelezwa kuwa uwezekano wa mahusiano kati ya Donald Trump na serikali ya Urusi, na badala yake Ijumaa iliyopita kutoa taarifa kwa bunge la Marekani-Congress za ujumbe wa kingono, katika uchunguzi wa Anthony Weiner, mbunge wa zamani wa New York na mume wa zamani wa msaidizi wake mkuu wa Clinton Huma Abdidin.
Katika taarifa hiyo Reid amemwambia kiongozi huyo wa FB kuwa jitihada za wazi kabisa zenye kuonesha ana nia ya kusaidia upande mmoja wa chama. Aidha ameongeza kuwa ofisi yake imemuandikia barua hiyo kwa kutanabaisha kuwa amekiuka sheria iitwayo "Hatch Act", ambayo inawazuia maafisa wa FBI kutumia mamlaka yao ya kiofisi katika kufanikisha ushawishi katika chaguzi. Amesema kwa kitendo cha kujiegemeza kwa upande wa chama amevunja sheria za taifa hilo.
Kutikisika mbio za Ikulu ya Marekani
Comey amezitikisa mbio za ikulu ya Marekani- White House kwa barua yake kwa Congress, akiwaeleza wabunge kupatikana kwa barua pepe mpya. Chama cha Democrat kina wasiwasi uvumbuzi huo mpya unaweza kumpa nguvu mpya mgombea wa Republican katika juma la mwisho kuelekea uchaguzi wa rais pamoja na kuwaongezea nguvu wagombea wa useneta na baraza la wawakilishi katika uchaguzi huo.
Katika hatua tofauti kufuatia kadhia hiyo mwanasheria mkuu wa zamani Eric Holder na waendesha mashitka wengine kadha wa kadhia wametia saini barua inayomkosoa Comey kutokana na kisa hicho cha hivi karibuni cha namna anavyoshughulikia tuhuma za barua pepe za mgombea Clinton.
Katika barua hiyo ambayo shirika la habari la Ufaransa la AP imeipata nakala yake inasema Comey amejitenga na kitenmgo cha sheria pale alipolidokeza bunge la Marekani juu ya uchunguzi mpya wenye kuhusiana na uchunguzi mpya kuhusiana na kashfa ya Clinton.
Aidha barua hiyo vilevile imeeleza maafisa wa Kitengo cha Sheria nchini humo wameagizwa wasiendelee kujadili uchunguzi unaondelea na kujitenga kabisa na jambo hilo katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, kwa lengo la kuondosha ushawishi wao. Lakini mkurugezi wa FBI alikwisha sema pale alipozungumza na maafisa wenzanke wa shirika hilo la ujasusi Ijumaa iliyopita kuwa barua yake kwa bunge la Marekani ipo katika hatari ya kutoeleweka katika kipindi hiki cha karibu na uchaguzi, lakini alipsawa kulipa taarifa bunge hilo baada ya awali kulieleza kuwa uchguzi wake ulifungwa. DW

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger