Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeanza mazungumzo na Taasisi ya
Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyoko Muhimbili, Dar es Salaam.
TFF
imeanza mazungumzo hayo, ili kwa pamoja waanze kushiriana kutoa mafunzo
kwa madaktari na wahudumu wa afya kwa wanamichezo wa soka katika
kushughulikia matatizo ya moyo.
Ni
matumaini yetu kuwa mafunzo haya yataboresha uwezo wa madaktari wa mpira
wa miguu sambamba na kusambazwa kwa vifaa maalumu vya tiba ya moyo
kwenye klabu za soka nchini.
Hii ni
hatua thabiti inayochukuliwa na uongozi wa TFF baada ya kutokea vifo
vinavyosababishwa na mshtuko wa moyo kwa wachezaji ukiwamo ugonjwa wa
‘cardiac arrest’ ambao kwa taarifa za AWALI unaonyesha ndio
uliosababisha kifo cha Mchezaji wa Mbao FC U20, Ismail Mrisho Khalfan.
Marehemu
Ismail Mrisho Khalfan alifariki dunia baada ya kuanguka uwanjani Desemba
4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera wakati timu yake ya Mbao
ikicheza na Mwadui katika mechi ya ligi ya vijana wenye umri wa chini ya
miaka 20.
Kifo
hicho kimegusa hisa za wanafamilia wengi wa mpira wa miguu akiwamo Rais
wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA), Bw.
Gianni Infantino ambaye juzi alituma salamu za rambirambi kwa Rais
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Emil Malinzi
kutokana na kilo cha ghafla cha Mchezaji.
Salaam
Rais Infantino, zinakwenda sambamba na za Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo wa Tanzania, Ndugu Nape Nnauye na Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou.
Mchezaji
Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20
wa Mbao FC ya Mwanza, kilitokea Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa
Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera wakati timu yake ikicheza mchezo huo dhidi
ya Mwadui FC ya Shinyanga.
Timu hiyo
ya Vijana wa Mbao, kama vilivyo timu nyingine 7 za Ligi kuu ya Vodacom,
ilikuwa Kituo cha Bukoba katika Ligi ya avijana ambayo kwa msimu huu
imefanyika kwa mara ya kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa kituo cha Dar
es Salaam.
Ismail
aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza uwanjani
hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani, lakini baadaye taarifa za
kitabibu zilionyesha amefariki dunia.
Kamati ya
Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha mchezaji huyo
kabla ya baadaye kutoa taarifa za kamili ya kitatibu kujua hasa chanzo
hasa cha kifo cha mchezaji huyo ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye
Hospitali ya Mkoa Kagera. Marehemu Ismail Mrisho Khalfan alizikwa
Desemba 5, 2016 jijini Mwanza.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment