Kutoka
kushoto ni Ibrahim Samuel- Meneja Uhusiano- Mikopo ya Nyumba, Wasia
Mushi- Naibu Mkurugenzi Benki ya Afrika Tanzania (BOA), na Muganyizi
Bisheko- Meneja Masoko Utafiti na Maendeleo wakiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani).
Kutoka
kushoto ni Beatrice Mirigo- Marketing executive, Ibrahim Samuel- Meneja
Uhusiano- Mikopo ya Nyumba, na Wasia Mushi- Naibu Mkurugenzi Benki ya
Afrika Tanzania (BOA) wakiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).
BANK OF
AFRICA- TANZANIA jana imezindua aina mpya ya mkopo wa ujenzi wa nyumba
unaoitwa ‘WEZESHA’ ambapo mtu anaweza kukopa kiasi cha shilingi milioni
40 hadi 500 kwa mrejesho wa miaka hadi 25 bila utaratibu wa kutoa malipo
yoyote ya awali.
Akizungumzia
progamu hiyo, Naibu Mkurugenzi wa BANK OF AFRICA- TANZANIA bwana Wasia
Mushi alisema, ‘programu hii ya mkopo wa ujenzi wa makazi mapya unawapa
uwezo wateja wetu kubuni nyumba zao kadiri wanavyopenda, kulingana na
mahitaji yao na ndani ya bajeti zao. Kwa kiwango kidogo kabisa cha riba
na katika viwango vya punguzo, Bank ya Afrika pia imetengeneza mazingira
rafiki na kuondoa usumbufu kwa mteja pindi anapohitaji mkopo huu’
Aidha,
huduma ya mkopo ya ‘Wezesha’ inapatikana kwa watu wote wenye mishahara
katika sekta za umma na binafsi, na kwa kutoa muda wa miaka 25 ya kulipa
deni, mkopaji atapata uhuru zaidi pindi atakapochukua mkopo.
Mpango wa
huu wa ‘Wezesha’ kujenga makazi unalenga kutoa suluhu kwa changamoto za
makazi zinazowakabili watanzania wengi ambao kwa mazingira ya kawaida
hutumia zaidi ya miaka 10-15 kujenga nyumba ya kawaida ya kuishi.
Fursa hii
ya kutatua changamoto ya makazi kwa watanzania wengi, inaendana na
ongezeko kubwa la watu kupata ardhi iliyopimwa, hivyo kuwapa watu nafasi
ya kujenga nyumba wanazozitaka kwa masharti nafuu na rahisi ambapo kwa
kuanzia mteja atatakiwa kuwa na kiwanja ambacho nyumba hiyo itajengwa.
Kwa
mujibu wa takwimu, Tanzania ina uhaba wa nyumba kwa ajili ya makazi
zaidi ya 3,000,000. Huku kukiwa na ongezeko la uhitaji huo kwa zaidi ya
asilimia 1 kila mwezi.
Muganyizi
Bisheko, Meneja Masoko Utafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA-TANZANIA
aliongeza kuwa, ‘Benki inatoa asilimia 100 ya ufadhili wa ujenzi ili
watu wengi waweze kuumudu mkopo. Mara nyingi, hasa kwa mtu anayeanza
maisha, kujiwekea akiba na kupata kiwango cha kulipia gharama za ujenzi
wa makazi ni jambo gumu sana. Jambo hilo liliwezekana kwa wale wenye
kipato kikubwa na endelevu, lakini kwa sasa, na kwa uwepo wa WEZESHA, si
jambo gumu tena la kuchelewesha ndoto zako za kumiliki makazi ya
kuishi, kwa kuweka akiba kwa miaka 2-5’
Aliongeza
kuwa, ‘Mara mteja wetu anapopata mkopo wa makazi, yeye ndiye atachagua
mkandarasi wa kujenga nyumba yake miongoni mwa makandarasi
waliochaguliwa na BANK OF AFRICA- TANZANIA. Mkopo utatolewa kulingana na
hatua za ujenzi, kama vile msingi, boma, paa, na umaliziaji. Na fedha
hizo zitapelekwa kwenye akaunti ya Kandarasi anayejenga iliyofunguliwa
kwenye Benki ya Afrika.Baada ya kukamilisha ujenzi, ripoti ya mkaguzi wa
ubora itakabidhiwa kabla ya fedha za hatua nyingine ya mkopo kutolewa’
Kwa mara
ya kwanza BANK OF AFRICA- TANZANIA ilizindua mkopo wa nyumba mwaka 2011
ambao ulikuwa unajumuisha mkopo wa ununuzi wa nyumba pamoja na
uboreshaji wa nyumba. Toka mkopo ulipoanza kutolewa zaidi ya shilingi
bilioni 10 zimeshatolewa.
Pamoja na
mikopo ya nyumba, BANK OF AFRICA- TANZANIA pia imekuwa ikitoa mikopo
kwa wakandarasi wa ujenzi ili kuongeza upatikanaji wa nyumba bora za
makazi na wakati huo huo wakiwezesha watu wa kawaida kuzinunua nyumba
hizo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment