Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam
kwa kushiriki katika zoezi la kuhakiki Namba ya Utambulisho Mlipakodi
(TIN).
Kutokana
na mwitikio mkubwa wa wananchi kutaka kuhakiki taarifa zao, Mamlaka
imeamua kuongeza muda wa uhakiki hadi tarehe 31 Januari, 2017. Pamoja na
kuongeza muda wa uhakiki, Mamlaka pia imeongeza vituo vya kuhakiki
TRA pia
inawakumbusha wananchi kuwa wale wenye TIN za biashara wanatakiwa
kuhakiki katika ofisi za kodi Mkoa husika na wenye TIN zisizo za
biashara (yaani TIN iliyotokana na maombi ya leseni ya udereva au ya
kuingiza mzigo bandarini) wanaweza kuhakiki katika kituo chochote hapa
Dar es Salaam.
Vituo vya uhakiki vilivyopo ni kama ifuatavyo:
Pamoja na
vituo hivyo, Mamlaka imeanzisha kituo kinachohama (Mobile Office)
ambacho kinatoa huduma sehemu mbalimbali. Ili kuongeza ufanisi, Mamlaka
itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza vitendea kazi na vituo
vingine vya kuhakiki.
Mwisho,
Mamlaka inawasihi wananchi kuepuka kutumia Matapeli (Vishoka) kwani
zoezi hili linamtaka mlengwa kufika mwenyewe kwenye kituo husika.
Kwa
ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa walipakodi
kwa kupiga simu za bure: 0800 780078 / 0800 750075 barua pepe: huduma@tra.go.tz
Pamoja Tunajenga Taifa Letu
Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao Makuu. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment