Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Filamu na Tamthilia za Kitanzania zitakazorushwa na DSTV kupitia Chaneli yao kuanzia Maisha Magic Bongo Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akizungumza katika
uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Mtendaji Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mkuu MNET, Yalisa Phawe akitoa hutuba fupi katika uzinduzi huo. Kulia
ni Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi.
Wadau wa filamu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali walioshiriki uzinduzi huo.
Wasanii wa filamu na wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Taswira katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) na viongozi wengine wakizindua Filamu na Tamthilia za Kitanzania.
Na Dotto Mwaibale
TANZANIA
imeingia katika mapinduzi makubwa ya tasnia ya filamu baada ya Maisha
Magic Bongo kwa kushirikiana na Multchoice Tanzania pamoja na maprodyusa
kuzindua rasmi chaneli yao (160) Maisha Magic Bongo itakayo kuwa
ilirusha filamu na tamthilia za kitanzania.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu na Tamthilia za kitanzania kwa
niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
ambaye alikuwa mgeni rasmi, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania,
Joyce Fissoo alisema mpango wa kurusha filamu za kitanzania kupitia
mtandao wa DSTV utasaidia sana kutangaza filamu zetu na kuleta ushindani
katika ulimwengu wa kimataifa.
“Serikali
tunaona hili ni jambo muhimu sana litakalowafanya wadau wa kazi za
kitanzania kutabasamu tena kwani sote tunafahamu umaarufu wa chaneli
zilizopo DSTV na jinsi zinavyoweza kuwafikia watu wengi duniani” alisema
Fissoo.
Aliongeza
kuwa uzinduzi huo uliohusisha filamu sita, tamthilia mbili na kazi
nyingine mbili DSTV wametoa mtaji wa dola za kimarekani 450,000.
Mkuu wa
Chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi alisema uzinduzi huo
umelenga kusherehekea kazi nzito za maprodyusa wa filamu hapa nchini na
utambulisho rasmi wa chaneli yetu yenye maudhui ya kitanzania.
Alisema
chaneli hiyo imelenga kuburudisha na kuelimisha watamazaji wa kitanzania
kupitia filamu, tamthilia na maigizo mbalimbali ya kiswahili.
Aliongeza kuwa chaneli hiyo itapatikana kwenye kifurushi cha huduma za DSTV (160).
Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe alisema DSTV Tanzania imetoa ajira 80 hivyo kusaidia katika maendeleo ya nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe alisema DSTV Tanzania imetoa ajira 80 hivyo kusaidia katika maendeleo ya nchi.
Mtendaji
Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage alisema mpango huo utasaidia kukuza
lugha ya kiswahili kama alivyokuwa akifanya mtunzi wa mashairi hayati
marehemu Shabani Robert katika kukuza lugha hiyo.
SHARE








No comments:
Post a Comment