TRA

TRA

Wednesday, May 17, 2017

MAMBO 15 USIYOFAHAMU YA KUSHANGAZA KUHUSU MBWA MWITU

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

1. Maisha yao ni mpela mpela, hakunaga muda wa kupumzika muda wa kazi kila kitu ni mchaka mchaka tuu, wanaharaka pasina mfano.
2. Wanaamini katika sera ya kiujamaa.
3. Ni marufuku kujipaka damu wakati wa kula, na atayepatikana na damu wenzie humtafuna pia.
4. Wanapokula hunyofoa nyama hula, hujifuta damu kisha hufata nyama tena.
5. Wanaokula hutenga chakula cha
watoto, sasa wewe na ukubwa wako jaribu kula utakoma.
6. Ukimpiga mmoja akakimbia dakika tano nyingi atarudi na kundi na utajuta kuzaliwa, 
Nyati huwa wanaelewa sana kinachowapata kwa sababu ya ubabe wao.
7. Hawa majamaa huwa hawakubali kushindwa, na kushindwa kwao ni kurudi nyuma kujipanga.


8. Hutambua wanyama wagonjwa na hutumia sana fursa hiyo kuwakamata hasa wale wakubwa kama nyati na twiga.


9. Ukiwaonyesha damu ni kama umewaharibu akili hapo hawatajali wewe ni nani, binadamu, simba , chui, nyati ukianguka ndio wanaridhika.


10. Ni wanyama ambao hutumia muda mfupi sana kuridhishana kimapenzi, dakika chache tuu Biashara imeisha na kibendi juu.


11. Huwaficha watoto wao wasiwaone wawapo katika mahaba, cha ajabu watoto wao mwaka mmoja tuu nao huanza kufanya waliyokuwa wamefichwa sasa sijui wanajifunzia ndotoni. 




12. Staili wanayotumia kula hata wanyama wanaokula nyama huishia kuwatizama tuu, na hakuna anayeweza kuwasogelea hata kama ana njaa, fisi huwa anachekaa weeee mpaka anaamua akafanye kazi nyingine.


13.Wakishiba muda wao mwingi hutumia katika michezo, mfano kupigana , kukimbizana nk.


14. Kachezee chochote alichonacho Ila ukitaka ubaya naye kaguse watoto wake na kama kamoja kambeya kapige kelele, jicho utalopigwa litasadifu unachokwenda kufanywa.


15. Jike hupandwa na dume mbabe, hivyo wanyonge wa mwisho huenda kutafuta majike katika koo zingine na huo huweza kuwawinda mwanzo wa kuanzisha jamii yao mpyaa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger