Na Nteghenjwa Hosseah - Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amewataka wafadhili na wadau wa watoto kubuni miradi inayoendana na kusaidia Mpango wa Serikali wa Elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari ili kupunguza changamoto zinazojitokeza kwa sasa na kuuwezesha mpango huu kutekelezwa kwa mafanikio makubwa.
Mhe. Gambo ameyasema
hayo wakati wa Mkutano wa kushirikishana tuliojifunza wakati wa
utekelezaji wa mpango wa pamoja tuwalee uliotekelezwa kwa miaka sita
kwenye Kanda ya Kaskazini na ambao kwa sasa umemaliza muda wake
ulifanyika kwenye Hotel ya Mt Meru Jijini hapa.
Akizungumza
katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa amesema kazi kubwa imefanyika wakati
utekelezaji wote wa mradi na mafanikio yake tumeonekana kwani watoto
wamefikiwa na kusaidiwa kutoka katika mazingira hatarishi yaliyokuwa
yanawakabili na wengine kupatiwa kadi za msamaha wa matibabu na zaidi
mradi huu umekabidhiwa kwa Halmashauri husika ambazo zitaendelea
kusimamia na kutekeleza mipango iliyowekwa chini ya mradi wa Pamoja
Tuwalee.
Aliendelea
kusema kuwa kukamilika kwa mradi huu katika awamu ya kwanza ni wazi
kabisa kwamba ni maandalizi ya mradi mwingine ambao utakua na malengo
yanayoshabihiana na programu ya awali hivyo ni vyema kwa kuwa walengwa
bado ni watoto niwatake wadau kubuni miradi utakaolenga kusaidia Elimu
bure na kwa kuwa watoto wote wanapata Elimu bure kupitia mpango huu basi
ni vyema mkaelekeza nguvu kwenye utoaji wa Chakula kwa wananfunzi suala
ambalo tumeona ni changamoto kwa watoto wetu.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la WEI – Bantwana “World
Education Inc” Bi. Gill Gap alisema wanajivunia kuwa Taasisi
iliyofanikisha utekelezaji wa mradi wa pamoja kwa ushirkiano wa Serikali
ya Tanzania katia utekelezaji wa mradi pamoja na Serikali ya Marekani
kwa ufadhili mradi huu. Pamoja Tuwalee ilikuwa maalumu kuwalinda watoto
walio katika mazingira hatarishi na kutoa Elimu kwa wazazi
walioathirika namna ya kuishi na watoto hao pamoja na kuwajengea uwezo
watumishi wa Halmashauri kuendeleleza jitahada za mradi huu.
Jacklin Badi ni
Mkurugenzi wa WEI – Tanzania anasema “Bantwana ni kitengo ndani ya
Shirika la WEI kinachohudumia watoto na hapa Tanzania tulianza
utekelezaji mwaka 2010 na mpaka sasa tumefanikiwa kuwafikia watoto
1,470,445 pamoja na wazazi wao na wameweza kupatiwa huduma jumuishi za
kuwasaidia na kuwalinda watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Naye
Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Wanawake, watoto na vijana “Center
for women, Children and Youth Development (CWCD) Bi. Hindu Ally Mbwego
ambao ni watekelezaji wa mradi huu wa Pamoja Tuwalee kupitia mwamvuli wa
WEI-Bantwana amesema wamefanikiwa kuwafika katika maeneo yote ya Jiji
la Arusha, Halmashauri ya Karatu na Moshi na wanajivunia mafanikio
waliyoyapata kutokana na mradi huu.
Tumebadilisha
maisha ya watoto na kuhakikisha usalama wao katika Jamii wanazoishi,
tumewatambua wazazi wenye watoto walioathirika na kuwapa elimu ya jinsi
ya kuwafahamisha watoto wenye hali hiyo na namna ya kuishi nao ili
waweze kukua katika malezi bora na afya njema sanjari na kupata Elimu
alisema Bi. Hindu.
Mradi wa pamoja Tuwalee ni mpango wa Kitaifa wa miaka mitano uliotekelezwa na fedha za mpango
wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupunguza makali ya virusi vya ukimwi
kwa waathirka kupitia Shirika la Misaada la Marekani la USAID na
kutekelezwa na WEI-Bantwana pamoja na Kituo cha maendeleo ya Wanawake, watoto na vijana kilichopo Jijini Arusha.
Mkurugenzi
wa WEI-TANZANIA Bi. Lilian Badi (aliyesimama) akielezea mafanikio ya
Mradi wakati wa Mkutano wa kuhitimisha mradi wa Pamoja Tuwalee.
Mkurugenzi
Mkuu wa World Education Inc Bi.Gill Garb akitoa taaria ya utekelezaji
wa mradi wa Pamoja Tuwalee kupitia WEI-Bantwana.
Mwakilishi wa US-AID Tanzania Bi. Maria Busquets akielezea namna ambavyo Shirika lake limefanikisha utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akizungumza na wadau wa Mkutano
Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Wanawake, watoto na vijana (CWCD) Bi. Hindu Ally Mbwego akielezea mafanikio ya mradi kupitia Kituo chake ambao ndio watekelezaji katika Halmashauri za Jiji la Arusha, Karatu na Moshi.
Picha
ya pamoja ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha (katikati mbele), Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi waliotekeleza mradi huu, viongozi wa WEI, US AID, CWCD
pamoja na Wadau wa watoto walioshirki katika Mkutano wa kuhitimisha
mradi wa Pamoja Tuwalee.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(mbele kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa CWCD Bi. Hindu Ally Mbwego (kulia mbele) pamoja na baadhi ya watoto wa Pamoja Tuwalee.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Pili kushito) kwenye picha ya pamoja na wadau waliotekeleza mradi wa Pamoja Tuwalee
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akiwa na wataalam kutoka
Halmashauri ya Korogwe waliofanikisha utekelezaji wa mradi wa Pamoja
Tuwalee.
SHARE
No comments:
Post a Comment