TRA

TRA

Saturday, November 19, 2016

PRIDE Tanzania Yatoa Misaada kwa Wateja Wake Walioathirika na Tetemeko la Ardhi Bukoba

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


PRIDE (Promotion of Rural Initiative and Development Enterprise)ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) linalotoa huduma za kifedha kwa masharti nafuu kwa wafanyabiashara ndogondogo na wa kati. Huduma hizo zina lengo la kuchangia pato la taifa na kuondoa umasikini nchini. 
PRIDE ilisajiliwa mnamo Mei 1993 chini ya wadhamini wasio na hisa (Company Limited by guarantee, not Having Share Capital) kulingana na Sheria ya Makampuni Cap, 212 ya mwaka 2012.na kuanza rasmi shughuli zake mwaka 1994 mjini Arusha.Kwa sasa Shirika lina matawi 85 yalioenea nchi nzima.
Tangu kuanzishwa, PRIDE imeweza kukopesha wajasiliamali mbalimbali nchini wapatao 1,700,000 nakutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni miatisa (bil. 900.0).
Katika kuungana naWatanzania, PRIDE Tanzania walitoa misaada mbalimbali moja kwa moja kwa wateja wao wa tawi la Bukoba ambao waliathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.Msaada huu ulilenga kuwawezesha wateja wa PRIDE kukarabati makazi yao. 
Vilevile PRIDE ilichangia katika mfuko wa maafa wa serikali kwa kutoa mifuko ya saruji na mabati.
pr1
Mtejawa PRIDE Tanzania,Tawi la Bukoba, Bw. Revocatus Siliden akifurahia msaada wa mifuko ya saruji aliyopewa kwa ajili ya kumsaidia katika ujenzi wa nyumba ya ke iliyoharibika baada ya kutokea tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
pr2
Mteja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba, Bw. Revocatus Siliden akionyesha madhara aliyoyapata kwenye nyumba yake baada ya kutokea tetemeko la ardhi huko Mkoani Kagera.
pr3
Afisa wa PRIDE Tanzania, Ndugu Samson Tenga akimkabidhi Mteja wa PRIDE Tanzania, Tawi la Bukoba mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yake ambayo ilibomoka kutokana na janga la tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr4
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Mstaafu Salum Kijuu akifurahia jambo na mmoja wa wawakilishi wa wateja wa PRIDE Tanzania, tawi la BukobaBi. Mariam Seleman ambae pia ni muathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr5
Diwani wa Kata ya Miembeni, Manispaa ya Bukoba, Mkoa wa Kagera (Shati la Kijani) Bw. Richard Gaspar pamoja na maafisa wa PRIDE Tanzania wakimkabidhi mifuko ya saruji mteja wa PRIDE, ambaye nyumba yake iliathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba.
pr6
Meneja wa Kanda ya Ziwa, Bi. Hilda Nsombo akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Mstaafu SalumKijuu msaada wa mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr7
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Mstaafu SalumKijuu akimshukuru Meneja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba Bi. Digna Tarimo baada ya kupokea msaada wa mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr8
Mmoja wa wateja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba, Bw. Audax John akionyesha nyumba yake jinsi ilivyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr9
Nyumba ya Bi.Dorosta Pastory mmoja wa wateja wa PRIDE Tanzania walionufaika na msaada wa saruji uliotolewa na PRIDE ikionekana upande wa nyuma baada ya ukuta wake kuanguka kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr10
Moja ya nyumba za wateja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba walionufaika na msaada wa saruji uliotolewa na PRIDE ikionekana upande wa mbele baada ya ukuta kuanguka kutokana natetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr11

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Mstaafu Salum Kijuu akimshukuru Meneja wa PRIDE Tanzania, Kanda ya Ziwa, Bi. Hilda Nsombo baada ya zoezi la upokeaji wa misaada ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera. Wengine ni Meneja wa PRIDEtawi la Bukoba, Afisa wa PRIDEtawi la Bukoba pamoja na viongozi wa wateja wa PRIDE tawi la Bukoba.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger