TRA

TRA

Monday, July 17, 2017

Mhenga alisema, ukitaka kula lazima ukubali kuliwa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Said Mwishehe

JUMAPILI ya leo naomba kabla ya kwenda mbali zaidi nitumie nafasi hii kutoa salamu zangu za dhati kwa wahenga. Shikamoni wahenga wetu.

Nieleze kidogo na kwa tafsiri rahisi ya mhenga ni nani au Wahenga ni watu wa aina gani?

Mhenga ni mtu mwenye hekima na busara katika kufanya jambo au kuliamua. Hivyo wahenga ni watu wenye busara na hekima ndani ya jamii na wengi wao ni wazee wetu.

Waliitumia misemo mingi katika kutafuta ufumbuzi wa jambo, au wakati mwingine kueleze kitu.Hawakuwa na parapara kwani waliamini unaweza ukasema na jamii ikaelewa unachomaanisha.

Hivyo wahenga waliitumia misemo kama sehemu ya njia ya kuendesha maisha yao kwenye jamii.

Kwa Ujinga Wangu wakati nikiendelea kutafakari misemo mingi ambayo imesemwa na wahenga nikamkumbuka Mhenga aliyesema ukitaka kula lazima ukubali kuliwa kidogo.

Namkumbuka kwasababu aliamini ili kufanya jambo lolote la maendeleo lazima kwanza fedha itumike ili kupata fedha nyingine.

Ahsante mhenga na kizuri zakidi Mungu anaendelea kumpa afya njema. Mungu naomba umpe afya njema mhenga wetu. Nakumbuka wakati anatoa msemo huo wapo ambao hawakumuelewa akawaambia "Sina maana hiyo".

Kwa Ujinga Wangu lazima nikiri misemo ya wahenga wetu imekuwa ikitumia tangu na tangu na kwa sehemu kubwa imekuwa na mafanikio makubwa.

Kuna migogori mingi ambayo inatokea kwenye jamii yetu lakini kwa kutumia misemo ya wahenga imesaidia kuepusha shari.

Kuna familia ambazo ziliingia kwenye migogoro kwa sababu tu ya kugombania mali lakini misemo ya wahenga na hasa ile ya 'Cha mtu mavi'.

Msemo huo maana yake ni moja tu kila mtu anatakiwa kutafuta cha kwake na si kutumia muda mwingi kujadili mali iliyotafutwa na mwingine.

Pia kwenye familia kuna wakati zinaingia kwenye matatizo tu hasa pale kunapoibuka kuwa mtoto aliyezaliwa si wa baba husika. Wahenga walitumia misemo ya 'Kitanda hakizai haramu' na kweli nyumba nyingi ndoa zikabaki kuwa salama.

Nani ambaye hakumbuki usemo wa hahenga unaosema 'Elimu haina mwisho'. Ukweli ni kwamba elimu haina mwisho na maana yao ilikuwa ni kusisitiza jamii kuendelea kuisaka elimu kila kukicha.

Unapomaliza hatua moja ya elimu unafuata na hatua nyingine na hivyo jamii kuwa na watu wenye uelewa mpana na maarifa. Shikamoni Wahenga wetu.

Kwa Ujinga Wangu natamani yale ambayo wahenga waliyasema yangekuwa kwenye kitabu kimoja na kisha kunzwa mahali ili ibaki kumbukumbu ya waliopo sasa na wengine.

Kuna hatari naiona ya kukosa maneno ya wahenga kwa miaka ya baadae. Misemo mengi ambayo inatumika sasa ni juhudi za wazee wetu ambao walilelewa kwenye misingi ya hekima na busara na wao wakaitumia busara hiyo kuwa na misemo ambayo leo hii tunaitumia.

Kwa Ujinga Wangu naona namna ambavyo kwenye mitandao ya kijamii, misemo ya wahenga ilivyoshika kasi na kila mmoja anaitumia kwa staili yake.

Kwenye mitandao ya kijamii ni kawaida kukuta imewekwa picha ya mtu na kisha unaambiwa huyu ndiye Mhenga alisema ukimuamsha aliyelala basi utalala wewe.

Kimsingi inaleta raha licha ya kwamba inatumika kama sehemu ya mzaha na kufurahishana mtandaoni. Kwanini raha?

Ni kwa sababu hata wale ambao hawakuwa wakifuatilia misemo ya wahenga leo hii wanafamu wazee wetu wenye hekima na busara walisema nini kwa ajili ya jamii yetu.

Ukweli ni kwamba kupitia mitandao ya kijamii hivi sasa kuna misemo mingi ya wahenga nimepata nafasi ya kuijua. Hata Mhenga aliyesema 'Ukubwa jalala' naye aliona mbali.

Ukubwa ni jalala na huo ndio ukweli kwani unapokuwa mkubwa kuna mambo mazuri na mabaya na yote yanakuwa kwako.

Kubwa na la msingi ambalo wengi wetu ni vema tukaweka akilini, kwenye mitandao tunayo nafasi ya kuitumia misemo ya wahenga kama sehemu ya utani na kufurahishana lakini tunaporudi kwenye uhalisia wake ni bora ikaendelea kutumika kwa malengo ambayo wazee wetu walikusudia.

Wahenga waliposema chanda chema huvishwa pete naamini walikuwa na maana anayefanya jambo nzuri anastahili pongezi.

Hivyo Wahenga nao wanastahili kupongezwa kwa mchango wao kwa Taifa.Hakuna jambo gumu kama kuacha msemo ambao utakuwa na faida kwa jamii yako.

Kwa Ujinga Wangu naamini Wahenga kwa kutumia misemo yao hakika walionya, walifundisha, waliekeleza na wakati mwingine kutoa angalizo.

Kwa mfano msemo wa Mhenga alisema 'Tafakari kabla ya kutenda'na hata aliyesema 'Kimfaacho mtu chake'.

Hakika kuna misemo mingi ya Wahenga ambayo kwetu itabaki kama dira na muelekeo pindi unapotaka kufanya jambo lolote liwe iwe kazini au katika shughuli binafsi.

Ahsante wahenga mliona mbali na nimekumbuka hata aliyesema 'Baniani mbaya kiatu chake dawa'

Kwa Ujinga Wangu kwa haraka haraka unaweza usiamini kuwa misemo hiyo kuna mahali imesaidia kututa jambo lakini nikushauri likikufika usione aibu, waza kisha kumbuka msemo wa Mhenga ambaye unaamini utakusaidia kwa wakati huo.

Wahenga walisema 'Asiyekubali kushindwa si mshindani. Kwa ule msemo unaosema 'Akufukuzae hakwambii toka' bila kufahamu msemo wa mhenga aliyesema 'Hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho.

Kwa maoni
0713833822
Mwisho

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger