Uzinduzi
wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini
ulitanguliwa na maandamano yaliyopita katika barabara mbalimbali za mji
wa Moshi na kuhitimishwa katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini
Moshi.
Washiriki
kutoka Asasi mbalimbali wakipita mbele na mabango yakiwa na ujumbe
mbalimbali katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
kanda ya kaskazini.
Baadhi
ya viongozi wa taasisi mablimbali wakiwa wameketi meza kuu na mgeni
rasmi wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya kaskazini Said
Mecky Sadiki.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia,Elizabeth Mushi
akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi
wa siku 16 za kupinga ukatli wa kijinsia.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Elizabeth Mushi
akipeana mkono na Mgeni rasmi katika unzinduzi huo,Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Said Mecky Sadiki mara baada ya kutoa taarifa juu ya
ukatili.
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki kutoa hotuba yake wakati wa
uzinduzi wa siku 16 za kupina ukatili wa kijinsia.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akizungumza wakati wa uzinduzi
wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ,uzinduzi iliofanyika katika
viwanja wa vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
Mwenyekiti
wa Mtandao wa Polisi katika Shule ya Polisi Theresia Nyangasa akisoma
taarifa juu ya vitendo vya kuutali na njia zilizoanza kuchukuliwa katika
kukabiliana navyo wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili
kanda ya Kaskazini .
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki pamoja na Mkuu wa wilaya ya
Moshi Kippi Warioba wakifuatilia taarifa juu ya ukatili wa kijinsia
iliyokuwa ikitolewa na viongozi wa Asasi mbalimbali .
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro akitoa cheti kwa Kaimu Kamnada wa Polisi mkoa wa
Kilimanjaro Koka Moita cha kutambua mchango wa jeshi la Polisi katika
kupamban vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akipena mkono kabla ya
kumkabidhi cheti Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF Network)
Grace Lyimo ,kutambua mchango wake katika vita dhidi ya ukatili wa
kijinsia.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akipeana mkono na Mwenyekiti
wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi wilaya ya Moshi,Elina Maro kabla
ya kumkabidhi cheti kutambua mchango wake katika vita dhidi ya ukatili
wa kijinsia.
Mkuu
wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya
washiriki alipopita kugagua mabanda ya maonesho ya shughuli zinazofanywa
na taaisisi zinazopambana na ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti
wa TAWREF ,Dafrosa Itemba akitoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili wa
kijinsia wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
kwa kanda ya kaskazini uliofanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha
mabasi mjini Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHARE
No comments:
Post a Comment