Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya mikopo ya Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa (kushoto), akimkabidhi Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Emelda Kisosi, kompyuta kwa ajili ya kusaidia ufanisi wa kazi ofisi zao kama sehemu ya kujitolea kwa jamii. Kulia ni Ofisa TEHAMA wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Edna Mwaipiana.
Na Mwandishi- Wetu, Arusha
HALMASHAURI ya Wilaya Arumeru, mkoani Arusha, jana imepokea kompyuta mbili zilizotolewa msaada
na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kama sehemu ya
ushirikiano na kusaidia na kukuza ufanisi wa kikazi kwa watumishi wa
umma wilayani humo.
Kompyuta hizo zinatoka ikiwa ni siku chache baada ya Mkoa wa Morogoro nao kupokea msaadakama huo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma.
Mratibu
wa Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial
Services inayojihusisha na mikopo, Mercy Mgongolwa katikati akizungumza
jambo katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Kulia ni
Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Emelda Kisosi.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo leo jijini Arusha, Mratibu wa Masoko na
Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema
wamefikisha kompyuta mbili katika wilaya
hiyo kama
orodha ya mahitaji waliyopokea kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Alisema anaamini kwa
kufikisha kompyuta hizo, kutachangia ufanisi wa kikazi kwa kutumia vyema
teknolojia ya kompyuta iliyokuja kupanua wigo wa utendaji bora wa kazi
kwa Tanzania nzima kwa hali ya kupanga, kutatibu na kuhifadhi kumbukumbu
muhimu za kiutendaji wakati wote.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya kompyuta hizo.
Mercy Mgongolwa akikabidhi nyaraka za kompyuta hizo.
“Huu ni mwendelezo mzuri wa ugawaji wa kompyuta 205 tulizonunua zenye thamani ya Sh Milioni 500, ambapo tayari kompyuta 125 zimefikishwa Makao Makuu ya Utumishi na wao kutuelekeza eneo na idadi ya ugawaji kwenye halmashauri za nchi yetu,” alisema.
Naye Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Imelda Kisosi, aliwashukuru Bayportkwa kujitolea vifaa hivyo muhimu vitakavyowapatia urahisi watendaji hao kuchapa kazi kwa nguvu zote ili wilaya yao isonge mbele.
“Msaada huu ni mkubwa mno kwetu hivyo tunawashukuru na kuwaahidi ushirikiano wa hali ya juu sanjari
na kuwataka Bayport waendelee kuwa karibu na jamii yetu kama njia ya
kuwapatia maendeleo Watanzania wote, hususan wa wilayani kwao Arumeru,
mkoani Arusha,” alisema Kisosi.
Bayport Financial Services ni taasisi ya mikopo inayojitolea kwa hali na mali ambapo mbali na kununua kompyuta hizo 205, pia imekuwa ikishiriki kujenga madarasa katika shule mbalimbali, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kupanua kiwango cha elimu nchini.
Huduma
znazotolewa na Bayport ni pamoja na mikopo ya fedha taslimu kwa
watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, mikopo ya viwanja,
mikopo ya fedha kwa njia ya simu za mikononi maarufu kama ‘Nipe Boost’,
Bima ya Elimu kwa Uwapendao na nyinginezo zinazopatikana katika ofisi
zao za matawi 82 katika mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania Bara.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment