Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru
akizungumza wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya Kwazna ya Viwanda vya
Tanzania yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam. Takribani Viwanda
vidogovidogo 362 vilishiriki katika maonesho hayo ya yaliyoanza kuanzai
tarehe 07 hadi 11 Desemba 2016.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Viwanda) Dkt.
Adelhelm Meru akipokea zawadi kutoka kwa Kikundi cha Sanaa cha Albino
Revolution Cultural Troupe kwa kuthamini mchango wake katika kukuza
uwekezaji kwa watuwenye ulemavu wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya
Kwanza ya Viwanda vya Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Viwanda) Dkt.
Adelhelm Meru akimkabidhi Cheti cha Ushiriki wa maonesho ya Viwanda vya
Tanzania mwakilishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. James Ndege
wakati wa hafla ya kufunga maonesho hayo jana jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendeji wa TANTRADE Bw. Edwin Rutageruka.
Baadhi
ya washiriki wa maonesho ya kwanza ya viwanda vya Tanzania wakifuatilia
hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji (Viwanda) Dkt. Adelhelm Meru alipokuwa akifunga maonesho hayo
jana jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Viwanda) Dkt.
Adelhelm Meru akipokea zawadi kutoka Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya maonesho ya viwanda vya Tanzania Bibi. Neema Mhondo
(kushoto) kwa kuthamini mchango wake katika kukuza viwanda nchini wakati
wa hafla ya kufunga maonesho hayo jana jijini Dar es Salaam.Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa rai kwa Watanzania kutumia
malighafi zinazopatikana nchini kwa ajili ya kuendeleza viwanda na
kukuza uchumi wa nchi.
Rai hiyo
imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji (viwanda), Dkt. Adelhelm Meru alipokuwa akifunga
Maonesho ya Kwanza ya Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tangu Disemba 7
mwaka huu katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo jijini humo.
Dkt. Meru
amesema kuwa nchi ya Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza viwanda na
kukuza uchumi wa nchi kutokana na uwepo wa malighafi za uhakika,
jiografia nzuri ya nchi kwa kuwa imepakana na nchi nyingi ambazo hazina
Bandari, miundombinu bora pamoja na rasilimali watu.
“Serikali
inafanya juhudi kubwa kuhakikisha viwanda vinaongezeka na kukua kufikia
viwanda vya kati na vikubwa hivyo nawaomba wananchi waendelee kutumia
malighafi za ndani kwani itawasaidia kupunguza gharama za uzalishaji wa
bidha zao na kupelekea kila mwanachi kuweza kununua bidhaa hizo kwa bei
rahisi,” alisema Dkt. Meru.
Katibu
Mkuu Meru ameongeza kuwa ili kuhakikisha ajira zinaongezeka nchini na
umasikini unapungua ni lazima kuwekeza zaidi katika ujasiriamali wa
viwanda vidogo ambavyo ndio mwanzo na chimbuko la viwanda vikubwa.
Aidha,
amewapongeza wajasiriamali kwa kutengeneza bidhaa zenye ubora na viwango
vya kimataifa pia amewasihi kufanya juhudi katika kutafuta soko la nje
ya nchi ili kuongeza pato la Taifa na kujenga uchumi wa nchi.
Naye
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE),
Edwin Rutageruka amesema kuwa kwa kiasi kikubwa malengo ya
maonesho hayo yametimia kwani kwa muda wa siku 5 wajasiriamali wamepata
semina mbalimbali zitakazowawezesha kuboresha biashara zao, wametangaza
bidhaa zao wanazozalisha pamoja na kupata fursa kwa wazalishaji
mbalimbali wa malighafi kuonana na wenye viwanda ili kuwauzia malighafi
hizo.
“Ingawa
malengo ya maonesho haya yametimia lakini bado kuna tatizo kwa
Watanzania kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kwetu, hivyo
tunawasihi wapende bidhaa zetu kwani viwanda haviwezi kuendelea bila
kuwa na soko la ndani la uhakika,” alisema
Maonesho
hayo yameandaliwa na Wizara ya Viwada, Biashara na Uwekezaji kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali, yamepangwa kufanyika kila mwaka kwa
nia ya kuitangaza sekta ya viwanda nchini pamoja na kutoa mafunzo
mbalimbali kwa wajasiriamali juu ya kuendeleza viwanda vidogo
walivyonavyo kufikia viwanda vya kati na vikubwa.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment