Waandishi
wa Habari walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa
ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakinyanyua
kuashiria kuanza safari hiyo atika lango la Marangu.
Safari
ya kupanda ikaanza katika lango la Marangu majira ya saa 5 asubuhi kila
mmoja akiwa na nguvu za kutosha na shauku ya kutzama madhari ya Mlima
Kilimanjaro ambao siku ya kwanza safari inaanza kwa kupita katika msitu
mnene.
Wapandaji
waliokuwa wamevalia nguo za kuzuia baraidi mapema wakati safari ya
kupanda mlima inaanza baadae kidogo kidogo walilazimika kuzipunguza kwa
sababu pindi unapotembea joto la mwili pia huongezeka.
Safari
ya kupanda mlima kwa kundi hili la Wanahabari na Askari wa jeshi la
Ulinzi (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,George
Waitara lilikuwa pia na ulinzi wa kutosha.
Hatimaye
safari kafika eneo la Kisambioni ikiwa ni nusu ya safari ya kuelekea
katika kituo cha Mandara ,eneo ambalo hutumika kwa ajili ya kupata
chakula.
Maeneo mengine Washiriki walilazimika kupumzika kwa ajili ya kupata nguvu mpya ya kuendelea na safari.
Majira
ya saa 12 jioni hatimaye Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku
ya kwanza ikafika katika kituo cha Mandara na washiriki wakapata nafasi
ya kupata picha ya pamoja na kupumzika kwa ajili ya siku ya pili
kuendele na safari ya kwenda kituo cha Horombo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya
Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment