Kundi la
kigaidi la Al Shabab nchini Somalia, limeshambulia kambi ya wanajeshi wa
Kenya katika eneo la Kulbiyow karibu na mpaka na nchi hiyo.
Msemaji
wa kundi la Al Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab amesema washambuliaji
wake wamefanikiwa kuwauawa wanajeshi 57 wa Kenya waliokuwa katika kambi
hiyo baada ya kuwashambulia Ijumaa alfajiri.
Hata
hivyo, jeshi la Kenya kupitia msemaji wake Luteni Kanali Paul Njuguna,
amekanusha madai ya wanajeshi wa KDF kuuawa na kusema kilichotokea ni
tishio la shambulizi ambalo halikufanikiwa.
Aidha, ameeleza kuwa jeshi la Kenya linapambana na wanamgambo hao na kuongezea kuwa wengi wao wametoroka.
Mwaka
uliopita, mwezi Januari kundi la Al Shabab walivamia kambi nyingine ya
KDF katika eneo la El Adde, na kusababisha vifo vya wanajeshi 100.
Jeshi la
Kenya linashirikiana na wanajeshi wengine kutoka mataifa mbalimbali ya
Afrika chini ya mwavuli wa AMISOM kupambana na kundi la Al Shabab ambalo
linataka kuiangusha serikali ya Mogadishu inayoungwa mkono na Jumuiya
ya Kimataifa.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment