Maafisa wa Idara ya Dharura na Askari polisi wametumwa karibu na makavazi ya Louvre, Ijumaa hii Februari 3.
Mwanjeshi wa Ufaransa anayelinda jengo la kihistoria la makumbusho
jijini Paris nchini Ufaransa, amempiga risasi na kumuua mwanaume
aliyejaribu kumshambulia askari aliyekuwa anapiga doria.
Ripoti zinasema kuwa, mwanaume huyo aliyekuwa anatamka Allahu Akbar alijaribu kutekeleza shambulizi hilo kutumia panga.
Waziri Mkuu Bernard Cazeneuve amesema mwanaume huyo alikuwa analenga kutekeleza shambulizi la kigaidi.
Baada ya jaribio hili, rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ni lazima kuwa makini kuhusu matukio kama haya.
Trump ametoa matamshi haya siku chache baada ya kuagiza kuzuiwa kwa wakimbizi kutoka mataifa saba za Kiislamu kuja nchini humo.
Ufaransa imekuwa katika hali ya
tahadhari baada ya mwaka uliopita, kushuhudia shambulizi la kigaidi na
kusababisha mauaji jijini Paris na Nice.
SHARE
No comments:
Post a Comment