Na Mathias Canal, Lindi
Mkuu
wa wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango ameitaka Halmashauri ya
Wilaya hiyo irejeshe maeneo yote ya wazi yaliyo vamiwa na kutumika
kinyume cha matumizi yaliyolengwa.
Dc
Muwango ametoa agizo hilo mjini Nachingwea kwenye uzinduzi wa kampeni
ya kitaifa ya kudhibiti magonjwa yasioambukiza na yanayoweza kuzuilika
kupitia mazoezi na michezo.
Uzinduzi
huo uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine ambapo Alisema
kuwa yeye kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo
anatambua na anazotaarifa za kutosha kuwa maeneo mengi ambayo yalitengwa
kwa ajili michezo na shuguli nyingine za umma yamevamiwa na
kubadilishwa matumizi.
Dc Muwango ameitaka halmashauri hiyo kurejesha haraka kutoka mikononi mwa wavamizi.
Katika
hali inayoonesha kuwa mkuu huyo wa Wilaya amelivalia njuga suala hilo,
ameitaka Halmashauri hiyo ipeleke na kumkabidhi mikakati na taarifa za
utekelezaji wa agizo lake haraka iwezekanavyo.
Sambamba na agizo hilo Muwango ameitaka Halmashauri hiyo kutenga maeneo kwa ajili ya michezo.
Amebainisha
kuwa bila kuwa na maeneo ya wazi itakuwa vigumu kufanikiwa kukuza
michezo na kuibua vipaji mbalimbali vya wanamichezo.
Amemuagiza
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwaandikia wakuu wa
shule za sekondari na walimu wakuu wa shule za msingi ili warejeshe mbio
za mchakamchaka kwenye shule zao kwani shule nyingi wanafunzi
hawakimbii mchakamchaka.
"Jambo
ambalo ni muhimu kwa afya na akili za wanafunz ila walimu wawe na
usimamizi mzuri ili wanafunzi wasiathiriwe katika masomo na usalama
wao," Alisistiza Muwango.
Akizungumzia umuhimu wa michezo na mazoezi Dc Muwango alisema kuwa licha ya kuimarisha, umoja,undugu na mshikamano.
Lakini pia mazoezi na michezo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo, utulivu na amani katika jamii.
Alibainisha
kuwa chanzo cha baadhi ya migogoro katika baadhi ya jamii ni magonjwa
ambayo yanaweza kuepukwa kwa kufanya mazoezi ambapo Hata hivyo jamii
husika hazitambui jbo hilo Badala yake inayahusisha magonjwa hayo na
sababu zisizo na msingi Ikiwa ni pamoja na Imani potofu, uchawi na
ushirikina mambo ambayo hupelekea kunyoosheana vidole na kusababisha
migogoro.
"Lakini
mtu akiwa mgonjwa hawezi kufanya shuguli za kiuchumi na maendeleo yake
mwenyewe, Taifa na hata wanaomuuguza hawawezi kufanya kazi ambazo
zingewaletea maendeleo," aliongeza Muwango.
Mkuu
huyo wa Wilaya alitoa wito kwa wananchi wilayani humo kujenga utamaduni
wa kufanya mazoezi bila kujali rika Huku akiwaasa kuunda vikundi vya
michezo na mazoezi Kwa sababu madhara ya kutofanya mazoezi ni makubwa
ambapo sio rahisi kuyabaini haraka.
Uzinduzi
huo ambao ni utekelezaji wa agizo la makamu wa Rais aliyetaka kuwe na
kampeni ya kitaifa ya kudhibiti magonjwa yasioambukiza na yanayozuilika
kupitia michezo uliandaliwa na ofisi ya mkuu huyo wa wilaya ya
Nachingwea Ambapo michezo mbalimbali ilichezwa, sambamba na upimaji wa
afya na uchangiaji damu kwa hiari.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango akisisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango akionyesha mfano wa ufanayaji mazoezi
Mkuu
wa wilaya ya Nachingwea ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama wa Wilaya hiyo Mhe Rukia Muwango akifanya mazoezi katika
uzinduzi huo
Matembezi yakiendelea vyema
SHARE
No comments:
Post a Comment