Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Selemani Jafo,amesema mkoa wa
Pwani umepokea Bil.2.340 zitakazotumika kugawanywa kwenye vituo vya afya
na zahanati 234 zilizopo mkoani hapo ili kuboresha na kutatua
changamoto zilizopo.
Amesema
fedha hizo zimetolewa kutoka katika mpango wa malipo kwa ufanisi
unaotekelezwa kwa ushirikiano baina ya bank ya dunia na serikali ya
Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.Aidha Jafo amewasihi
wakurugenzi,wenyeviti wa halmashauri na mganga mkuu wa mkoa
huo,kusimamia fedha hizo ili ziweze kuleta tija .
Katika
hatua nyingine,ametoa wiki moja hadi kufikia februari 21 mwaka huu,kwa
waganga wakuu wa mikoa (RMO)na makatibu tawala wa mikoa (RAS)kote
nchini,kuhakikisha wanapeleka account za bank zinazotumiwa katika vituo
na zahanati zote.Alhaj Jafo,aliyasema hayo wakati akizungumza na
wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri pamoja na waganga wakuu wa
wilaya mkoani Pwani.
Alisema
kati fedha hizo kila zahanati na kituo cha afya kitapatiwa kiasi cha
sh.mil 10 ili kuboresha na kutatua kero sugu zilizokuwa
zikiwasumbua.“Kuna zahanati na vituo vya afya ambavyo havina
magodoro,mapaa yamebomoka,,hakuna vyoo huku nyumba za mganga wa kituo
nayo ikiwa haina choo”“Kuna maeneo mengine hayana hata vitanda vya
kujifungulia,akinamama wanapata shida yaani unahofia wanaweza kuondoka
hata na magonjwa mengine,hivyo kwa mazingira haya fedha hizi endapo
zitatumika kikamilifu zitaondoa matatizo hayo”alisema Jafo.
Alisema
katika miaka iliyopita fedha hizo zilikuwa hakuna hivyo kutokana na
mpango huo kuanza,wahakikishe wanaleta matokeo chanya kwa kujibu
changamoto zilizokuwa zikiwakabili.Jafo alisema hatofurahishwa akisikia
mradi huo haujafanikiwa katika mkoa wa Pwani na mikoa mingine 8 ambayo
ipo kwenye mradi huo kwa majaribio hapa nchini.
Akizungumzia
suala la utoaji huduma bora za kiafya,alieleza kuwa ni tatizo kubwa na
aibu kwani katika mkoa huo jumla ya vituo 153 vina nyota 0(0 star)kati
ya vituo 234 vilivyopo .Alifafanua kuwa vituo vinavyokosa star kubwa
ndivyo vinavyokosa mapato zaidi kwani endapo hospitali inafanya vizuri
inapata mil.360,kituo cha afya mil.79.8 na zahanati mil.19.
“Hili
ni tatizo la nchi nzima,niwaombe waganga wakuu wa wilaya na mikoa
kusimama kidete,kuhakikisha mnaondoa hizi 0,sifuri hizi hazina maana
,zinashusha mapato,kuanzia sasa mfanye juhudi mpate nyota 4 hadi
5”alisema Jafo.Alimtaka mganga mkuu wa mkoa wa Pwani,dk Beatrice
Byarugaba,kuacha kukaa ofisini badala yake atoke kutembelea vituo na
zahanati mbalimbali ili kujiridhisha na huduma inayotolewa.
Wakati
huo huo, Jafo alitoa wiki moja kwa makatibu tawala wa mikoa na waganga
wakuu nchini kupokea account zote za vituo na zahanati zilizopo kwenye
mikoa yao .Waziri huyo alisema endapo mkoa wowote utashindwa kutekeleza
agizo hilo basi katibu tawala na mganga mkuu wa mkoa husika watatakiwa
kutoa maelezo.
Nae
mchumi idara ya afya kutoka TAMISEMI,Nassoro Shemzigwa,alisema mpango
huo unatekelezwa katika mikoa tisa ikiwemo
Pwani,Shinyanga,Mwanza,Simiyu,Geita,Kagera na Mara .Alielezea kuwa lengo
la mradi ni kuboresha huduma za afya ya msingi kuanzia hospital ya
wilaya,zahanati na vituo vya afya.Shemzigwa alisema mpango huo
utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2015/2016 hadi
2020 na utakuwa ni endelevu.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Kibiti,Khatibu Chaurembo,alibainisha
wamepokea maagizo na maelekezo waliyopewa na wataenda kuyafanyia
kazi.Chaurembo aliiomba serikali kuangalia tatizo la uhaba wa watumishi
katika zahanati mbalimbali hasa maeneo ya vijijini ambako zipo zahanati
zenye mtumishi mmoja hivyo kusababisha huduma kuzorota.
NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Selemani Jafo,akizungumzia na
wakurugenzi,wenyeviti wa halmashauri,waganga wakuu wa wilaya mkoani
Pwani,jana.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
SHARE
No comments:
Post a Comment