Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza
mmoja wa washiriki katika kikao cha kuandaa Kanuni za Local Content.
Wengine katika picha ni wenyeviti wa Bodi za Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakuu wa
Mashirika pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na
Madini na Taasisi zake na wawakilishi wa kampuni za Wachimbaji wa Mafuta
na Gesi Asilia Nchini.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisikiliza
mada kuhusu Local Content iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix
Mgamlagosi (hayupo pichani). Wengine ni washiriki walio hudhuria kikao
hicho mjini Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Ntalikwa (wa pili
kulia) akiendesha kikao cha kujadili Kanuni za Local Content kwa niaba
ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Wengine ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BG, Marc Hartog (wa kwanza Kulia)
Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),
Profesa Sufiani Bukurura (wa tatu kulia), Kaimu Kamishna wa Nishati na
masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (wa nne kulia), Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Modestus
Lumato (wa tano kulia) pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya
Nishati na Madini.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisikiliza mada
kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji (EWURA), Felix Mgamlagosi (hayupo pichani). Kutoka
kushoto, Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC), Profesa Sufiani Bukurura, wa pili ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Profesa James Ntalikwa na wa tatu Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya BG, Marc Hartog wakiwa katika kikao hicho mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),
Felix Mgamlagosi (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kuhusu mada zilizotolewa
kwenye kikao cha kujadili Kanuni za Local Content kwenye Ukumbi wa
Wizara ya Nishati na Madini mjini Dodoma. Wanaofatilia ni Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) pamoja na
Wenyeviti wa Bodi za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakuu wa Mashirika na Viongozi
Waandamizi kutoka Wizarani.
Washiriki wa kikao cha Local Content wakifatilia kikao kilicho jadili Kanuni za Local Content mjini Dodoma.
………….
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Wachimbaji
wa Mafuta na Gesi Asilia nchini, Wenyeviti wa Bodi za Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Wakuu wa
Mashirika pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na
Madini na Taasisi zake ili kujadili Kanuni za Local Content kikao hicho
kilifanyika tarehe 11-12 mjini Dodoma.
SHARE
No comments:
Post a Comment