DRC yalalamika kwa Umoja wa Mataifa kuhusu M23
Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika Umoja wa Mataifa
ameeleza kwamba kuibuka upya kwa uasi wa kundi la M23 Mashariki mwa nchi
hiyo kunahatarisha makubaliano yaliofikiwa kati ya serikali na
upinzani. Katika barua yake kwa rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa, balozi huyo wa Kongo Ignace Gata Mavita, ameainisha msururu wa
matukio ya uvamizi wa M23, ulioanza Novemba mwaka uliopita na kuongezeka
mwezi Januari. Alisema hali hiyo itailazimu serikali kutumia fedha
nyingi kukabiliana na vita hivyo. Balozi Mavita amefahamisha juu ya
hatari inayoweza kuvuruga makubaliano ya kisiasa na mchakato mzima wa
uchaguzi nchini Kongo. Rais Joseph Kabila anapaswa kuachia madaraka
baada ya uchaguzi chini ya makubaliano hayo.
No comments:
Post a Comment