Taasisi
ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa
kushirikiana na Wakfu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA)
wamewakutanisha wabunge pamoja na waandishi wa habari leo katika ukumbi
wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Mkutano huu ulikuwa na lengo la kuwajengea
Wabunge na Wanahabari uhusiano mzuri katika utendaji wao wa kazi. Bunge
na Vyombo vya Habari ni Mihimili miwili ya dola (Mmoja ukiwa Rasmi na
mwingine usio Rasmi) inayotegemeana sana katika utendaji wake wa kazi.
Kutokana
na kazi kubwa ya Bunge ambayo ni kutunga sheria na kuwakilisha Umma
katika mijadala mbalimbali ya maendeleo katika ngazi za Taifa na Jimbo
lazima kutumia vyombo vya Habari kwenye kazi ya kutafsiri mipango na
mikakati mbalimbali inayofanywa na Bunge katika lugha ambayo mpiga
kura/mwananchi wa kawaida anaweza kuelewa. Lengo kuu likiwa ni
kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima.
Katika
siku za karibuni kumetokea changamoto mbalimbali katika utendaji kazi
wa muhimili huu rasmi na muhimili huu usiokuwa rasmi, na hasa
kutoaminiana na kushutumiana kwa namna moja ama nyingine. Kutokana na
changamoto hizo hakuna budi kwawaandishi wa habari paamoja ili kujadili
changamoto na kuja na suluhisho la changamoto hizo.
Semina
hiyo imeshirikisha watu 55 ikiwa ni pamoja na wabunge mbalimbali toka
vyama vyote, Wahariri wa vyombo Habari vilivyoko Dodoma na Bureau Chiefs
wa vyombo vya Umma na Binafsi vilivyopo Dodoma.
Mhariri
Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu
namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya bunge na wanahabari kwa
baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari katika ukumbi wa
Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na Geofrey Adroph.
Afisa
Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza
jambo mbele ya baadhi ya wabunge pamoja na baadhi ya wahariri na
waandishi wa habari waliofika katika semina ili kujadili jinsi ya
kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge na wanahabari yatakayoleta
ukaribu kwa pande zote.
Baadhi
ya wabunge wakichangia mada kuhusu kutengeneza mahusiano ya kikazi kati
ya Bunge(wabunge) na wanahabari pamoja na kutoa maoni yao ili kuboresha
utoaji wa habari kwa wananchi boila kujali itikadiza kivyama.
Mhariri
Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akijibu maswali kutoka kwa
wabunge katika mkutano uliowakutanisha wabunge, wahariri na waabdishi wa
habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.
Mhariri
mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitolea ufafanuzi baadhi ya
maswali yaliyoulizwa na waandishi pamoja na wabunge walioudhuria
mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.
Mmoja wa waandishi wa habari akitoa changamoto anazozipata kwenye kazi zake za kila siku za kuripoti habari mbalimbali
Baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari wakiwakwenye mkutano
SHARE
No comments:
Post a Comment