Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Bunda Bi. Janeth Mayanja amemvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Bunda B, Bw. Laurent Agustino kwa tuhuma za kushiriki kusaidia
mwanafunzi mmoja kufanya udanganyifu katika mtihani wa darasa la nne.
Mwalimu huyo anatuhumiwa kumruhusu
mwanafunzi wa darasa la tano kufanyia mtihani wa mwanafunzi wa darasa
nne kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi huyo ambaye hajui kusoma wala
kuandika ili aweze kufaulu.
Mkurugenzi huyo ametoa kauli hiyo leo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi.
Kufuatia tukio hilo Bi. Janeth ametoa
onyo kwa walimu wote wa shule zilizofanya vibaya na kuwataka kufanya
vizuri katika matokeo ya mitihani kwa mwaka 2017 na kuahidi kuwavua
madaraka walimu wa shule zitakazofanya vibaya.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bunda amewataka walimu wakuu, waratibu na walimu wote
kutekeleza kutekeleza majukumu yao kulingana na sheria na kanun9 a
utumishi wa Umma.
Mkurugenzi huyo amezizawadia shule
kumi za Msingi zilizofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza Darasa la
saba kwa mwaka 2016 kwa ajili ya kuboresha kiwango cha elimu katika
eneo hilo.
Utaratibu huo ulenga kutoa hamasa kwa
wanafunzi na walimu wilayani humo na kuongeza juhudi katika kufundisha
na kujifunza kwa ajili ya kuongeza kiwango cha ufaulu katika Halmashauri
hiyo.
Amezitaja shule zilizoingia kumi bora
ni pamoja na Olympus, Daystar, St. Paul, Mzuma, Kabarimu B, Bigutu,
Bukore, Kung’ombe, Kabarimu A na Bitaraguru ambazo zote zimetunukiwa
vyeti vya kutambua mchango na juhudi wanazofanya.
Mayanja alisema kuwa kati ya shule hizo
nne ni shule binafsi na sita za Serikali ambazo ambapo pamoja na
zimekabidhiwa hundi za fedha.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment