Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
JAJI
Mkuu anatarajia kupokea orodha ya majina ya mahakimu na majaji
ambao wamevuga kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za
kulevya.
Hayo
ameyasema leo Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini
Rogers Sianga wakati wa mkuatano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na
waandishi wa habari ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda kwa ajili kupambana na dawa za kulevya.
Sianga amesema
kuwa kesi zimevurugwa na mahakimu na majaji. hivyo wale wote
wanaohusika watashitakiwa na hata wawe na mali ambazo wamezipata kwa
biashara hiyo zitataifishwa.
Amesema
kuwa watazunguka katika maeneo mbalmbali ya jiji la Dar es Salaam ili
kuhakikisha mtandao huo unapatikana na kwenda hata Zanzibar na mbinu
zote wanazijua katika kufanya biashara hiyo.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemkabidhi orodha ya
majina 97 wanaojihusisha na dawa za kulevya na kuongeza kuwa moto
umewashwa dhidi ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.
Amesema
kuwa kuna nyumba 200 zinajihisisha na kufanya biashara ya madawa ya
kulevya hapa jijini ambapo wote hao watafikiwa katika operesheni.
Nae
Mohamed Khalid TID , amesema kuwa sasa ni mnyama ambae yuko tayari
kupambana nawatu wanaouza pamoja na kutumia dawa za kulevya na amerudi
kwa kufanya kazi na kuongeza kuwa kuimba hakuitaji dawa za kulevya.
Katika mkutano huo watu wawili wametakiwa kufika katika Kituo cha Polisi kati ambao ni Chidi Mapenzi, Ayuob Mfaume Kiboko.
SHARE
No comments:
Post a Comment