Mwanafunzi wa Iran Benham Prtopour baada ya kuruhusiwa na idara ya uhamiaji nchini Marekani kuelekea Boston
Jaji mmoja wa Marekani amesimamisha kwa
muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia kutoka
mataifa saba, yaliyo na raia wengi wa imani ya Kiislamu kuingia nchini
Marekani.
Jaji wa Seattle alipuuzilia mbali sababu
zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri hiyo inaweza
kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa mahakamani.
Serikali inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.
Serikali ya Marekani inasema kuwa makumi
ya maelfu ya visa zimefutiliwa mbali tangu rais Trump kutia sahihi amri
ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa kuingia nchini Marekani juma
lililopita.
Wakati huohuo waziri Mkuu wa zamani wa
Norway, Kjell Magne Bondovik, alisema kuwa alizuiwa katika uwanja mmoja
wa ndege mapema juma hili, katika tukio alilosema ni la uchokozi, kwa
sababu eti alikuwa na visa ya Iran katika paspoti yake.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment