Na Eliphace Marwa, Dar es salaam
Chama
cha Wakandarasi Tanzania kimeiomba Serikali kuwashirikisha katika zabuni
za ujenzi wa miradi mbalimbali ya umma Wakandarasi wazawa.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama hicho,
Mhandisi Lawrence Mwakyambiki wakati mkutano na waandishi wa habari
kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali katika sekta ya
ujenzi hapa nchini.
Alisema
kuwa wanaiomba Serikali ya Awamu ya Tano kuwashirikisha wakandarasi wa
kitanzania , wakimemo wakandarasi wa madaraja yote ili waweze kujijengea
kitaalamu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo
ujenzi wa majengo mbalimbali ya Serikali mkoani Dodoma.
Mhandisi
Mwakyambiki aliongeza kua hatua hiyo itasaidia kuongeza ajira kwa
vijana na Kampuni za kitanzania katika shughuli za ujenzi hapa nchini.
Aidha,
Chama hiyo kimeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa mstari wa
mbele katika kutekeleza mikakati na kusimamia sekta ya ujenzi hapa
nchini.
Aidha
Mwakyambiki aliongeza kuwa kutokana na uamuzi wa Serikali ya Awamu ya
Tano kuhamia Dodoma ni vema wakandarasi wa ndani wakapewa fursa ya
kushiriki katika kandarasi mbalimbali ambazo serikali inatarajia
kuzifanya huko Dodoma.
Kwa
upande Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi John
Bura alimshukuru Rais Magufuli na Serikali yake kwa kuitikia wito wa
wakandarasi kwa kuwatengea miradi michache ambayo ilikwisha tangazwa.
Aliwataka wakandarasi kuunda umoja kwa ajili ya kuitekeleza kwa weledi ili kuongeza imani kwa Serikali.
SHARE
No comments:
Post a Comment