Wanaume watatu
wamekamatwa kufuatia mauaji ya watangazaji wawili wa kituo cha Radio
waliokuwa hewani katika Jamuhuri ya Dominika.
Kanda ya video imeonyesha matangazo hayo yakikatizwa ghafla na kisha mwanamke mmoja anasikika akilia "Risasi! Risasi! Risasi!"
Polisi wamethibitisha shambulio hilo lilifanyika hapo Jumanne katika eneo la San Pedro de Macoris, mashariki mwa mji mkuu wa Santo Domingo.
Mwanamke mmoja alijeruhiwa na anaendelea kupokea matibabu
Wanaume waliokamatwa hawajafunguliwa mashtaka na polisi wanasema hawajui kilichosababisha mauaji hayo na kuongeza uchunguzi unaendelea.
Hapo mwezi Agosti mwaka 2015, waandishi habari wawili wa Marekani walipigwa risasi na kuuawa wakati wakitangaza kwenye runinga katika jimbo la Virginia.
SHARE
No comments:
Post a Comment