Mkurugenzi
Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza leo jijini Dar es salaam
katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la
‘Zantel Madrasa’ ambayo itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu
kujifunza kuhusu imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia
simu zao za mkononi. (Katikati) ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Aboubakar Zubeiry ambaye alikuwa mgeni rasmi na Mkuu wa Itifaki BAKWATA
Mohammed Nassor.
Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akizungumza mapema leo jijini
Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel
iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa
dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata
mafundisho kupitia simu za mkononi ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa
Zantel watakaopenda kutumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma
ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo. (katikati) ni
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Mkuu wa kitengo cha huduma na
bidhaa Zantel Hamza Zuheri.
Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel
Benoit Janin wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’
kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma hiyo uliofanyika mapema leo jijini
Dar es salaam.
Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa
vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es
salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’
itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel ikiwa ni mahususi kwa waumini
wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata
mafundisho kupitia simu za mkononi.
Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa
vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es
salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’
itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel mahususi kwa waumini wa dini
ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho
kupitia simu za mkononi. (Katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit
Janin pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Bw. Hamza
Zuheri.
Mwandishi
wa gazeti la The Citizen Alawi Masare (Kushoto) akifanya mahojiano na
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha
mawasiliano Zantel Rukia Iddi Mtingwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa
huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini
ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho
kupitia simu za mkononi.
Waumini
wa dini ya Kiislamu sasa watajifunza masuala ya dini kupitia simu za
mkononiZantel kwa kushirikiana na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA)
imezindua huduma mpya inayojulikana kama ‘Zantel Madrasa’ ambayo
itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza kuhusu imani ya dini
hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu zao za mkononi.
Huduma
hiyo itajumuisha mambo mbalimbali kama vile Hadithi, Quran, Dua na
huduma nyingine nyingi kupitia ‘App’ kwenye simu ya smartphone
((IVR/SMS/Mobile App and Bakwata News), ambapo pia mteja ataweza kupata
taarifa kwa kupiga simu.
Akizungumza
wakati wa sherehe ya uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es Salaam
leo, Ofisa Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema, “Tunafuraha
kuzindua huduma hii ya ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawaunganisha waumini wa
dini ya Kiiislamu nchini na kuwawezesha kupata maarifa ya dini hiyo kwa
urahisi zaidi.”
Kwa
upande wake Sheikh Mkuu wa BAKWATA, Mufti Abubakar Zuberi ambae alikua
mgeni rasmi alisema, “Hii ni huduma ya kipekee kwa jumuiya ya Waislamu
na kila mtu anayependa kujifunza kuhusu dini ya Kiislamu. Nawaomba
Waislamu wenzangu kutumia fursa hii mpya na mjiunge kwa wingi ili kujua
mambo yanayopaswa kufanywa katika Uislamu.”
“Ninaamini
kwamba huduma hii mpya itarahisha kazi kwetu viongozi wa Kiislamu kwa
kuwa mafundisho mengi yatakuwa yanapatikana kupitia Zantel Madrasa,”
alisema.
Aliongeza kwamba BAKWATA itaisaidia Zantel kuitangaza huduma hiyo hapa nchini Tanzania hususan katika misikiti.
Zantel
Madrasa ni huduma ya kwanza kuzinduliwa kwenye mitandao ya simu nchini
Tanzania ikilenga kutoa mafundisho ya dini na kuwaunganisha watu
kujifunza kuhusu dini nchini.
Huduma
hii inatoa fursa kwa Waislamu wote kujiunga na huduma hii kwa kupitia
namba maalumu za mtandao wa Zantel, hivyo kuwezesha watumiaji wa simu
zaidi ya milioni 1 kupata mafunzo ya Madrasa kwa siku.
Watumiaji
wa mtandao wa Zantel ambao watapenda kuitumia huduma hii watatakiwa
kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata
maelekezo utakayopewa ili kuunganishwa na kufurahia huduma hii.
SHARE
No comments:
Post a Comment