
Mabingwa watetezi wa Kombe la FA la Wanawake nchini Uingereza, Kina dada wa Arsenal, wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu.
Hii ni baada ya kuchapwa 1-0 na kina dada wa Birmingham City katika hatua ya robofainali.
Bao la Birmingham lilifungwa na Marisa Ewers dakika ya 77.
Kipa wa Birmingham Ann-Katrin
Berger alifanya kazi ya ziada kuwazuia Arsenal kufunga. Aliokoa
makombora kutoka kwa Kim Little, Danielle Carter na Danielle van de Donk
kipindi cha kwanza.
Katie McCabe na Jordan Nobbs
walishambulia lakini wakashindwa kulenga vyema wavu upande wa Arsenal
muda mfupi kabla ya Ewers kufunga.
SHARE
No comments:
Post a Comment