Chama cha Mapinduz (CCM) kimeelezea kuwa kamili katika
kuelekea kwenye mkutano wake maalum hapo
keshokutwa Machi 12 mwaka huu mjini Dodoma.
Tayari maeneo
mbalimbali ya mji wa Dodoma umeanza
kupepea bendera za Chama hicho cha Mapinduzi huku shamrashamra za hapa na pale
zikitarajia kunoga zaidi kuanzia leo Machi 11 na siku ya mkutano
wenyewe.
Kwa sasa mji wa Dodoma umekuwa na pilikapilika za hapa na pale huku
Ulinzi na usalama ukiwa umeimarishwa na wa hali ya juu hasa ikizingatiwa kuna
ugeni mkubwa ikiwemo wa wajumbe kutoka kila kona ya nchi nzima na viongozi wa nchi.
Awali akizungumza katika makao makuu ya CCM Mjini hapa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri
Kuu ya CCM, Humphrey Polepole amesema maandalizi yote yamekamilika na tayari wajumbe wamefika na wanaendelea
kufika huku vikao maalum vikiendelea kufanyika ni vile vya ndani
“Maandalizi yote yamekamilika ya mkutano wetu wa hapa
Dodoma. Kwa sasa CCM imeanza safari madhubuti na kuongeza tija katika
kuisimamia serikali katika ushahuri na maelekezo. Mkutano huu unakuja kuweka
uhalali na kuja kusimika mageuzi haya rasmi kikatiba. Mkutano huu utakuwa rasmi
kama chama cha Wanachama na kitashughulika na shida za wanachama na umma wa
watanzania.” Ameeleza Polepole.
Humphrey Polepole ameweka wazi kuwa, licha ya kuwa, halmashauri kuu ina uwezo wa
kupitisha mabadiliko hata hivyo wao
kupitia Mwenyekiti (Rais John Magufuli) Wameamua kuitisha mkutano wa dharura
ili kupitisha mabadiliko hayo.Polepole amesema mabadiliko yatasaidia kufanya mageuzi
makubwa na chama kurejea kwa wananchi wote na katika misingi imara
Aidha,
mikutano ya awali inatarajia kuanza
mapema ikiwemo ule wa Kamati Kuu ya CCM uliotarajia kufanyika jana Machi 10 huku
ule wa Halmashauri Kuu ukitarajia kufanyika leo Machi 11 na mwisho
mkutano huo wa Machi 12.
Kwa uzoefu wa mikutano hiyo mikuu ya Kichama hasa ya CCM, inapofanyika mjini hapa,
pamekuwa na wingi wa watu huku nyumba za wageni karibu zote zinakuwa zimejaa,
Hali kwa mkutano huu huenda ikawa na changamoto kwani kwa sasa tayari baadhi ya
watumishi wa Serikali hasa baadhi ya Wizara kuhamia Dodoma kama Makao makuu ya
nchi,
karibu nyumba nyingi za wageni wamekuwa wakizikodisha hivyo
kwa muingiliano wa mkutano huu changamoto hiyo inaweza kuwa maradufu kwa muda
hasa kwa kipindi hiki cha mkutano.
Na Andrew Chale-Dodoma
SHARE
No comments:
Post a Comment