Meneja wa SIDO Mkoa wa Mtwara Joel Chidabwa Akizungumza Machache wakati Akizindua Rasmi mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa Mtwara akiwa wa Wawezeshaji kutoka Taasisi Ya Manjano Foundation
Meneja
wa SIDO Mkoa wa Mtwara Joel Chidabwa kawataka wanawake wa Mkoa wa
Mtwara kuchangamkia fursa ya ujasiraiamali inayotolewa na Taasisi ya
Manjano Foundation. Amesema hayo mapema mkoani Mtwara alipokuwa
akifungua mafunzo hayo kwa wanawake wajasiriamali katika sekta ya
vipodozi na urembo. Mafunzo hayo yanatolewa bure kwa wanawake 30
waliotuma maombi na kuchaguliwa na Taasisi ya Manjano Foundation.
Akieleza
zaidi amesema “Shekha Nasser ni moja ya wawekezaji wa ndani ambao
wanapaswa kuungwa mkono kwani ameamua kuwekeza na kuwawezesha wanawake
kiuchumi kwa kutumia bidhaa za LuvTouch ambazo zimesajiliwa hapa hapa
nchini kuwawezesha wanawake kupata elimu ya ujasiriamali ili waweze
kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia bidhaa hizo”
Baada
ya kuhitimu mafunzo haya washiriki hao wataunganishwa na Taasisi za
kifedha ili kuweza kupata mikopo ya kupata mitaji ya kuanzisha bishara
Mwezeshaji Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation Bi Ester Lukindo Akizungumza Machache wakati wa Uzinduzi Huo .
Bi Ester Lukindo aliyesoma hotuba kwa niaba ya afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na Muasisi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama “Shekha Nasser alisema kuwa "wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka taasisi hiyo wanaweza kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye tasnia ya Urembo."

Washiri wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi.
Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka huu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi Mtwara ukiwa ni mkoa wa tatu tayari kufikiwa.
Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka huu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi Mtwara ukiwa ni mkoa wa tatu tayari kufikiwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment