SERIKALI ya Gambia imesema itaanzisha tume ya ukweli na maridhiano
kufuatilia uhalifu uliofanywa na utawala uliopita na itahakikisha
wahanga wa uhalifu huo wanalipwa fidia. Waziri wa sheria wa nchi hiyo
Abubacarr Tambedou alitanga hatua hiyo jana. Serikali ya Rais wa sasa
Adama Barrow iliahidi kufanya marekebisho ya maamuzi mengi yaliyofanywa
na aliekuwa Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh ambaye anashutumiwa na
makundi ya haki za binadamu kwa maamuzi yake ya ukiukaji wa haki za
binadamu dhidi ya wapinzani wake kisiasa. Gambia, taifa dogo la Afrika
Magharibi hivi sasa linaendelea kuchukua hatua kuhakikisha kuwa misingi
ya sheria inaheshimiwa nchini humo na mwezi uliopita maafisa tisa wa
zamani wa idara ya usalama wa taifa walikamatwa na kushitakiwa kwa
tuhuma za mauaji ya mwanaharakati mmoja wa upinzani. Waziri wa sheria
Tambedou amesema tume hiyo ya ukweli na maridhiano iataundwa katika
kipindi cha miezi sita ijayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment