TRA

TRA

Friday, March 24, 2017

Mapambano kuukomboa mji wa Raqqa kuanza

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
MAPAMBANO dhidi ya kundi linalojiita dola la Kiislamu ya kuukomboa mji wa Raqqa nchini Syria huenda yakaanza katika kipindi cha siku kadhaa zijazo amefahamisha hii leo waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yve Le Drian.

 Akizungumza na kituo cha televisheni cha Cnews waziri huyo amesema nchi yake siku zote imekuwa ikisema kwamba Raqqa ni lengo kubwa kwao na kwamba mapambano ya kuukomboa mji huo yanaweza kuanza siku kadhaa zijazo. 

Ameongeza kusema mapambano hayo yatakuwa makali ingawa ni muhimu sana. Mapema wiki hii wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema kwamba muungano wa kijeshi unaokabiliana na kundi hilo unaoongozwa na Marekani kwa mara ya kwanza uliwadondosha kwa ndege wanajeshi wa nchi kavu kuingia katika maeneo ya kuwazunguka maadui kwa upande wa nyuma karibu na mji unaodhibitiwa na kundi hilo la IS wa Tabqa kaskazini mwa Syria, katika hatua inayofungua mapambano mapya katika operesheni ya kuukomboa mji wa Raqqa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger