Maonyesho ya biashara yanayohusisha
makampuni mbalimbali kutoka nchini Mauritius yamezinduliwa leo jijini Dar es
Salaam yakilenga kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa
baina ya nchi hizo mbili kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara
baina yao.
Maonyesho hayo ya siku mbili yameratibiwa
na kampuni ya Talemwa Investment Consulting Company (TICC) ya nchini Tanzania, kwa
kushirikiana kampuni za Enterprise Mauritius (EM) Mauritius na apex Trade
Promotion Organisation Mauritius za nchini Mauritius huku yakihusisha zaidi ya
makampuni yaliyojikita kwenye sekta za kilimo, uhandisi, nguo na usafi kutoka
nchini Mauritius.
Akizungumza kwenye warsha fupi ya
uzinduzi wa maonyesho hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa TICC, Bw. David Lutabana
alisema maonyesho hayo ni fursa ya kipekee itakayowakutanisha wafanyabiashara
kutoka nchi hizo mbili ili kuweza kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili fursa
za kipekee zilizopo baina ya nchi hizo.
“Mauritius ni miongoni mwa nchi ambazo
zinakuja juu kwa kasi kiuchumi na zinaweza
kuwavutia wawekezaji kutoka nchini Tanzania kwenda kuwekeza kule wakati
huo huo tunatarajia kwamba Tanzania ikiwa kama kitovu cha biashara na maliasili
mbalimbali inaweza kuwavutia pia wawekezaji kutoka Mauritius kuja kuwekeza
huku,’’ alisema.
Aliongeza kuwa katika maonyesho hayo
ambayo pia yatatoa fursa kwa wahusika kujifunza tamaduni tofauti na zile za
mataifa yao, mada mbalimbali zitawasilishwa sambamba na mikutano kadhaa baina
ya wahusika kutoka pande hizo mbili.
Akizungumzia maonyesho hayo Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wafanyabiashara chini, Johnson Minja alitoa wito kwa
wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kutafuta fursa mbalimbali za kibiashara ili
kujiongeze masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini.
“Uwepo wa maonyesho haya ni wazi
utaendelea kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa kitanzania kuweza kutambua fursa
mbalimbali za kibiashara zilizopo nje ya nchi. Lakini pia maonyesho haya
yatafungua milango kwa wenzetu kutoka Mauritius kutuletea mawazo na mbinu mpya
kibiashara. Nawasihi sana wafanyabiashara wa Kitanzania wachangamkie sana fursa
hii,’’ alisisitiza.
Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Wafanyabiashara chini, Johnson Minja akizungumza kwenye
warsha fupi ya uzinduzi wa maonyesho
biashara ya Mauritius yaliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yanayohusisha
makampuni mbalimbali kutoka nchini Mauritius yanalenga kutoa fursa kwa wafanyabiashara
wadogo, wakati na wakubwa baina ya nchi hizo mbili kujenga mahusiano na
kutizama fursa za kibiashara baina yao
Ofisa Biashara Mkuu wa Tantrade, Stephen
Kobro akizungumza kwenye warsha fupi ya
uzinduzi wa maonyesho biashara ya Mauritius yaliyozinduliwa leo jijini Dar es
Salaam. Maonyesho hayo yanayohusisha makampuni mbalimbali kutoka nchini Mauritius
yanalenga kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa baina ya
nchi hizo mbili kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina yao.
SHARE
No comments:
Post a Comment